IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 4

Surah An-Nisa; Sura ya Qur'ani inayowaangazia wanawake

14:08 - June 09, 2022
Habari ID: 3475355
TEHRAN (IQNA) – Nafasi ambayo mwanamke anayo katika jamii na familia ni miongoni mwa masuala muhimu katika Uislamu. Dalili ya umuhimu huu inaweza kuonekana katika Sura ya nne ya Qur'ani Tukufu kama ilivyowekwa wakfu kwa wanawake.

Surah An-Nisa imeteremshwa Madina na inatilia maanani zaidi masuala ya kijamii. Sura hii ina aya 176 na ipo katika Juz nne hadi sita za Quran.

Imeitwa Nisa (wanawake) kwa sababu ina sheria nyingi kuhusu wanawake. Neno "Nisa" limerudiwa mara 20 katika sura hii.

Miongoni mwa mada muhimu zaidi za majadiliano katika Sura hii, tunaweza kuashiria kuharamishwa kwa unyakuzi wa mali za wanawake (aya ya 19-21), aina tofauti za wanawake na sheria kuhusu ndoa nao (aya 127-130), na tofauti za kisheria kati ya wanaume na wanawake (32-35). Sura pia inazungumzia sheria kuhusu ndoa na mirathi huku pia ikitaja baadhi ya nukta kuhusu swala, jihadi, na kushuhudia.

Qur'ani inataja idadi kubwa ya haki za wanawake ambazo hazikujulikana wakati huo. Mmoja wao ni kutambua haki za kifedha za wanawake.

Sura inasisitiza kulinda familia kama sehemu muhimu zaidi ya kijamii huku pia ikielezea ndoa kuwa ni jambo linaloweza kulinda jamii.

Zaidi ya hayo, Surah An-Nisa inarejelea hadithi mbili muhimu za kihistoria; moja wapo ni kuhusu kiapo cha Shetani cha kumpoteza mtu (aya 118-120) na nyingine ni kuhusu upotofu wa Waisraeli kama vile kumwomba Musa awaonyeshe Mungu, ndama wa dhahabu, mauaji ya manabii, na mashtaka dhidi ya Hazrat Maryam (SA).

Sura hiyo pia inawatahadharisha waumini juu ya njama na uadui wa maadui, ikibainisha haja ya kuwa na utayari wa kila kitu na kukabiliana na maadui katika nyanja mbalimbali.

Habari zinazohusiana
captcha