IQNA

Harakati za Qur'ani

Vyuo vikuu vya Iraq vyandaa Maonyesho ya Qur’ani Tukufu

22:03 - February 27, 2023
Habari ID: 3476632
TEHRAN (IQNA) – Maonesho ya Qur’ani Tukufu yamezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Alkafeel katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq.

Kituo cha Qur'ani cha Najaf chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya  Hadhrat Abbas (AS) itasimamia maonyesho hayo.

Maonesho hayo yamezinduliwa Februari 27 na kuendelea hadi Jumatano, Machi 1, kulingana na tovuti ya alkafeel.net.

Sayyed Zayd al-Ramahi, afisa wa idara hiyo, alisema maandalizi yote yamefanyika kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo la Qur'ani.

Aliongeza kuwa maonesho kama hayo yataandaliwa katika vyuo vikuu vingine kama vile Chuo Kikuu cha Kufa, Chuo Kikuu cha Ufundi cha Al-Furat AL-Awsat, Chuo Kikuu cha Imam Jafar Sadiq (AS), na Chuo Kikuu cha Tiba cha Jabir ibn Hayyan.

Shughuli za Qur'ani zimeendelea kwa kiasi kikubwa nchini Iraq tangu kupinduliwa kwa dikteta wa zamani Saddam Hussein mwaka 2003.

Kumekuwa na mwelekeo unaokua wa programu za Qur'ani kama vile mashindano, vipindi vya kisomo, maonyesho na programu za elimu zilizofanyika katika nchi hiyo ya Kiarabu katika miaka ya hivi karibuni.

3482618

Kishikizo: iraq qurani tukufu
captcha