IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran

Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi saba kutembelea maonyesho ya Qur’ani ya Tehran

21:48 - March 14, 2023
Habari ID: 3476703
TEHRAN (IQNA) - Mkuu Duru ya 30 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran amesema mawaziri wa wakfu na utamaduni wa nchi saba watatembelea tukio hilo la Qur'ani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hapa mjini Tehran siku ya Jumatatu, Ali Reza Moaf alisema maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi wa Sala  wa Imam Khomeini (RA) kuanzia tarehe 1-15 Aprili katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika maonyesho ya mwaka huu kutakuwa na kikao cha kuwaenzi watumishi wa Qur'ani, ambacho kitahudhuriwa na Rais wa Iran Ebrahim Raeisi, aliongeza.

Kwa mujibu wa Moaf, wale wanaoitumikia Quran katika nyanja nane maalumu wataeneziwa katika mkusanyiko huo.

Wakati wa hafla katika maonyesho hayo, Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri ya Qur'ani pia kitazinduliwa, alisema zaidi.

Pia alibainisha kuwa eneo linalotolewa kwa maonyesho hayo limeongezeka kutoka mita za mraba 50,000 za mwaka jana hadi mita za mraba 75,000 mwaka huu.

Akirejelea kipengele cha kimataifa cha maonyesho hayo, Moaf alisema nchi 22 zimetangaza utayarifu wa kushiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani na mawaziri wa wakfu na utamaduni wa nchi 7 pia watatembelea maonyesho hayo.

Amelinukuu Baraza Kuu la Mapinduzi ya Utamaduni likisema kuwa, maonyesho hayo ni tukio kubwa zaidi la Qur'ani Tukufu nchini Iran na ni miongoni mwa matukio makubwa ya Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu

4127881

Habari zinazohusiana
captcha