IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu Austria wanakumbana na chuki dhidi ya Uislamu

13:51 - March 30, 2023
Habari ID: 3476783
TEHRAN (IQNA)- Shirika moja lisilo la kiserikali imeripoti kuwa, wanawake Waislamu wanaovaa vazi la staha la Hijabu nchini Austria wanakabiliwa ubaguzi na mashambulio ya wenye chuki dhidi ya Uislamu ikilinganishwa katika nchi hiyo ya Ulaya.

Munira Mohamud, mwanaharakati wa Shirika la Dokustelle huko Austria ameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, zaidi ya matukio 1,000 ya chuki dhidi ya Waislamu yaliripotiwa mwaka jana nchini humo, huku wanawake wanaovaa Hijabu wakiwa wahanga wakuu wa kesi hizo ikilinganishwa na wanaume.

Maelezo ya kina ya utafiti wa shirika hilo lisilo la kiserikali kuhusu visa vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vilivyosalijiliwa mwaka jana 2022 yanatazamiwa kutolewa mwezi Mei mwaka huu.

Hata hivyo takwimu za asasi hiyo ya Dokustelle zinaonesha kuwa, asilimia  69.2 ya wanawake Waislamu walikabiliwa na hujuma za kibaguzi na chuki kutokana na imani yao mwaka 2021.

Mohamud, mkazi wa Vienna, na mmoja wa wanawake Waislamu walioshambuliwa kwa kuvaa Hijabu mwaka jana anasema, "Mwanamme mmoja alinikabili nilipokuwa nje, akaniliuza, nini hii umevaa kichwani, ivue!"

Hata hivyo, sio uhalifu wa mitaani pekee unaotekelezwa, ambao unawalenga Waislamu. Mvutano mkali wa 2021 ulidaiwa kuchochewa na serikali yenye utata iliyotekeleza "Ramani ya Uislamu," iliyoanzishwa na mamlaka ili kufanya upelekelezi na ujasusi katika misikiti yote kote Austria. Wakosoaji wanaamini kuwa sera hii ilichangia kuchochea  kuenea kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu.

Aidha Novemba 2020, mamlaka ya Austria ilizindua Oparesheni Luxor, ambayo ilishuhudia nyumba na ofisi za mashirika ya kutoa misaada ya Kiislamu na wanaharakati zikivamiwa kama sehemu ya kile kinachoitwa vita dhidi ya "Uislamu wa kisiasa." Kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali ya Austria, kuna Waislamu wapatao 645,600 katika nchi hiyo ya Ulaya. 

3482983

captcha