IQNA

Kongamano la ‘Vyombo vya Habari na Njia ya Fikra ya Soleimani’

23:32 - January 03, 2021
Habari ID: 3473520
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la kitaalamu la "Vyombo vya Habari na Njia ya Fikra ya Suleimani" lililofanyika leo katika Ukumbi wa Makongamano ya Kimataifa wa IRIB hapa mjini Tehran.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mhandisi Abdulali Ali-Asgari Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa dhihirisho la imani, taqwa na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na alifanya jitihada uhai wake wote katika kushikamana na njia ya fikra ya Imam Khomeini na Ayatullah Khamenei.

Mhandisi  Asgari ameongeza kuwa, Shahidi Soleimani, iwe ni wakati alipokuwa akihudumu kama kamanda shujaa, muumini na mwenye ikhlasi katika vita vya miaka minane vya Kujihami Kutakatifu, au wakati alipokuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alichukua hatua kubwa na za kistratejia kwa ajili ya Muqawama wa Kiislamu.

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Iran amebainisha kuwa, kamanda Suleimani alikuwa muumini na alichukua hatua kivitendo kulingana na misingi ya imani yake; na Mwenyezi Mungu alimfungulia njia na kumtunukia riziki isiyokwisha.

Akihutubia washiriki wa kongamano hilo, Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha IRIB Dkt. Peyman Jebeli ambaye pia ni mkuu wa kamati ya kielimu ya kongamano hilo la "Vyombo vya Habari na Njia ya Fikra ya Soleimani" amesema kamanda Qassem Soleimani alikuwa na ushujaa, ujasiri, uelewa, uwezo wa kutabiri na uono wa mbali wa mambo; na kwamba sifa hizo zina umuhimu mkubwa mno kwa mtazamo wa vyombo vya habari.

Kitabu cha maisha ya Shahidi Qassem Soleimani, alichoandika yeye mwenyewe kiitwacho "Nilikuwa Sihofu Chochote" kimezinduliwa pembizoni mwa kongamano hilo.

3945363

captcha