Naibu Kamishna Jenerali wa Magereza Nicholas Maswai ametoa agizo la moja kwa moja kuhusiana na hilo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa msikiti katika gereza la Machakos, afisa huyo wa umma huku akieleza kuwa kituo msikiti huo umejengwa kwa fedha za wafadhili, alitoa hoja ya kutenga ardhi ili kuhakikisha wafungwa wanapata chakula cha kiroho wanachohitaji.
Hatua hiyo, kwa mujibu wa Maswai inawiana na sera ya jumla ya serikali ya kurekebisha na kuboresha hali ya haki za binadamu katika vituo vya kurekebisha tabia.
"Idara ya Magereza la Kenya iko tayari kutoa ardhi kwa wafadhili wanaotaka kujenga misikiti," alisema wakati wa hafla hiyo.
Maswai aliendelea kueleza kuwa wasimamizi wa magereza wanatazamia kuajiri viongozi zaidi wa dini mbalimbali ili kushughulikia mahitaji ya kiroho ya wafungwa na maofisa wa serikali wanaotumikia katika vituo vya kurekebisha tabia.
Alitaja kuajiriwa kwa wahubiri wa Kiislamu mnamo 2021 kama hatua katika mwelekeo wa kuunganisha mageuzi ya kiroho kama sehemu ya urekebishaji tabia na ujumuishaji wa wafungwa katika jamii.
Katika hafla hiyo hiyo, Maalim Mkuu wa Magereza ya Kenya Sheikh Abass Makter, ambaye ni mhubiri mkuu wa Kiislamu katika huduma ya magereza aliahidi uungwaji mkono wake kikamilifu kuhakikisha kuwa msikiti mpya uliofunguliwa unaoitwa Masjid Yussuf utahudumia jamii ya magereza ipasavyo.
Sheikh Makter alisema msikiti huo utatumika kama nafasi ya kutafakari kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza.
3489815