Mashindanoo hayo ambayo hujulikana rasmi kama Mkusanyiko wa Kimataifa w Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Malaysia (MTHQA) yalianza tarehe 5 Oktoba katika Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Kuala Lumpur.
Jumla ya wasomaji na wahifadhi 92 kutoka nchi 71 wanashiriki katika mashindano hayo.
Mwakilishi wa Iran anaonekana kuwa mshindani wa mwisho kuwasili Malaysia baada ya kuchelewa mara kadhaa kwa safari za ndege kutokana na hali ya taharuki Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
Safari zake za awali za ndege siku ya Jumatano na Ijumaa zilikuwa zimekatishwa na kulikuwa na wasiwasi kwamba hangeweza kufika kwenye ukumbi wa mashindano kwa wakati.
Lakini hatimaye aliondoka Tehran siku ya Jumatatu na kufika Kuala Lumpur Jumanne asubuhi, Oktoba 8.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege, alifahamu kuhusu zamu yake ya kufanya usomaji wake, ambayo itakuwa Alhamisi jioni, Oktoba 10.
Maqari wa Iran wameshinda idadi kubwa zaidi nafasi za juu katika mashindano hayo maarufu la Qur'ani.
Miongoni mwa Wairani waliowahi kuchukua nafasi za juu katika mashindano hayo ni marehemu Mohammad Taqi Morovvat, Abbas Salimi, Ali na Msoud Sayyah Gorji, Abbas Emamjome, Mansour Qasrizadeh, Ahmad Abolqassemi na Mohsen Hajihassani Kargar, ambaye baadaye alikufa shahidi katika mkasa wa Mina mwaka 201. .
Mwaka jana, Ali Reza Bijani wa Iran alimaliza wa pili katika toleo la 63 la mashindano ya kimataifa.
3490193