IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Sashambulio dhidi ya mwanamke Mpalestina aliyevaa Keffiyeh Marekani

20:48 - October 20, 2024
Habari ID: 3479620
IQNA - Shambulio dhidi ya mwanamke aliyevaa keffiyeh (skafu ya kichwa ya Wapalestina) huko Brooklyn limelaaniwa huku kukitolewa wito wa mashtaka ya uhalifu wa chuki kwa wausika.

Mnamo Jumapili, Oktoba 13, takriban saa saa mbili unusu usiku, mwanamke mwenye umri wa miaka 38 aliripotiwa kushambuliwa huko Crown Heights, Brooklyn, New York mwanamke ambaye alikuwa amevalia keffiyeh. Imedokezwa alishambuliwa na wanawake wawili. Wahusika wanadaiwa kumpiga mwathiriwa ngumi usoni na kumsukuma chini.
Katika mapambano hayo, wanawake wote watatu walipata majeraha madogo. Maafisa wa Idara ya Polisi New York (NYPD) waliwakamata washukiwa hao haraka, na wamefunguliwa mashtaka ya shambulio lisilofaa.
Tawi la New York la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR-NY) limelaani shambulio hilo.
Katika taarifa yake, Wakili wa CAIR-NY Christina John alisema:
“Mitaa yetu lazima iwe sehemu salama kwa kila mtu, na tumejitolea kuhakikisha haki inatendeka. Tunashukuru vyombo vya sheria kwa kuwakamata haraka wahusika na kuwataka wajumuishe mashtaka ya uhalifu wa chuki. Keffiyeh inahusishwa na utambulisho wa Palestina na, kulingana na ripoti, utambulisho huo ndio ulichochea shambulio hilo. Mashambulio kama haya hayawezi kuvumiliwa kamwe."
Mapema wiki hii, CAIR-NY ililaani kitendo cha kuchomwa kisu kwa mchuuzi wa mikokoteni ya Halal.
Kuanzia Januari hadi Juni 2024, CAIR ilirekodi malalamiko 4,951 ya mashambulio ya chuki didi ya Waislamu kote Marekani, ongezeko la asilimia 69 katika kipindi kama hicho mnamo 2023.
Mapema mwaka huu, ofisi ya kitaifa ya CAIR ilitoa ripoti yake ya haki za kiraia ya 2024, ambayo ilifichua idadi kubwa zaidi ya malalamiko ambayo imewahi kupokea katika historia yake ya miaka 30. Ripoti hiyo ilisajili malalamiko 8,061. Karibu nusu ya malalamiko yote yaliyopokelewa mnamo 2023 na yaliripotiwa katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka, ikimaanisha chuki  dhidi ya Waisamu iliongezeka  baada ya Israel kuanza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina Gaza.

3490349

Habari zinazohusiana
Kishikizo: palestina cair
captcha