IQNA

Malamiko 5,156 ya hujuma dhidi ya Waislamu Marekani yalipokewa mwaka wa 2022

14:02 - April 13, 2023
Habari ID: 3476861
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR) lilitoa ripoti Jumanne iliyoangazia matukio ya kitaifa ya malalamiko ya haki za kiraia yaliyofanywa na Waislamu Wamarekani mwaka 2022 ambayo yalionyesha kupungua kwa 23%.

Mwaka jana, CAIR ambayo hutetea haki za  Waislamu ilipokea malalamiko 5,156 kote katika nchi hiyo.

"Malalmiko yamepungua kwa asilimia 23 kwani kulikuwa na malalamiko 6,720 ambayo CAIR ilipokea    mwaka 2021," ilisema ripoti hiyo, yenye kichwa "Maendeleo katika Kivuli cha Ubaguzi."

CAIR ilibaini kuwa pia ni mara ya kwanza kurekodiwa kupungua tangu waanze kufuatilia matukio ya chuki dhidi ya Uislamu mnamo 1995.

Malalamiko hayo yalihusisha aina mbalimbali za ubaguzi pamoja na matukio yanayohusu sheria, elimu na michezo.

Data hizo zilijumuisha ubaguzi wa mashirika ya ndege, ubaguzi wa benki, uonevu, kunyimwa huduma, ubaguzi wa elimu, ubaguzi wa ajira, kuhojiwa na FBI, uhalifu wa chuki na makabiliano na maafisa wa polisi.

Ripoti hiyo pia ilibainisha kuwa malalamiko kuhusu maafisa wa polisi na kubughudhiwa na maafisa wa kiserikali yalipungua kwa 38%. Wakati huo huo, malalamiko kuhusu matukio ya shule yaliongezeka kwa 63%.

Kulingana na Naibu Mkurugenzi wa Kitaifa wa CAIR Edward Ahmed Mitchell, takwimu zinaonyesha maendeleo na "changamoto kubwa" katika mapambano   kukabiliana na ubaguzi dhidi Waislamu.

Aidha aliserma, "Kuna ongezeko kubwa la 63% la malalamiko yanayohusiana na shule na ripoti za juu za ubaguzi wa ajira, matukio ya upendeleo na dhuluma za serikali zinahusu sana."

CAIR ilizitaka mashirika ya serikali, makampuni na jumuiya za mitaa kutekeleza hatua zilizopendekezwa katika ripoti yao ili kufikia maendeleo ya kudumu katika kuendeleza haki kwa wote, ikiwa ni pamoja na Waislamu wa Marekani.

3483179

Habari zinazohusiana
Kishikizo: cair waislamu marekani
captcha