IQNA

Waislamu Marekani

Malalamiko baada Meya Muislamu wa New Jersey, Marekani kuzuiwa kuingia Ikulu

17:51 - May 20, 2023
Habari ID: 3477023
TEHRAN (IQNA) – Mameya kumi na sita katika jimbo la New Jersey walionyesha kumuunga mkono Meya Muislamu Mohamed Khairullah, ambaye hakualikwa kwenye dhifa ya Idul Fitr iliyoandaliwa na Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House mapema mwezi huu.

Mameya walitangaza "barua ya mwito wa kuchukua hatua" katika programu iliyoandaliwa katika Msikiti wa Dar al Islah huko Teaneck, New Jersey.

Barua hiyo iliyotumwa kwa Mkurugenzi wa Huduma ya Siri ya Marekani Kimberly Cheatle na Katibu Msaidizi wa Biden wa Masuala ya Kijamii Carloz Elizondo ilisema wanamuunga mkono na kusimama na Meya Mtarajiwa Mohamed Khairullah, ambaye hakuruhusiwa kuhudhuria mapokezi ya Mei 1 dakika za mwisho kwa sababu za usalama.

Mameya hao walisisitiza kuwa "orodha ya washukiwa" ya FBI ni kinyume cha sheria ambayo ina watu milioni 1.5, wengi wao wakiwa Waarabu na Waislamu.

“Tunakuomba utoe sababu muhimu za kwanini Meya Khairullah alikataliwa kwenye mapokezi na umuombe radhi,” ilisema barua hiyo.

Ilisisitiza kwamba Khairullah ndiye Meya Muislamu aliyekaa muda mrefu zaidi katika New Jersey akiwa na miaka 17 madarakani na kutaka kuondolewa kwa "orodha ya washukiwa" ya serikali, ambayo inajumuisha Khairullah, ambaye amebaguliwa isivyo haki na kubaguliwa.

Khairullah alitoa changamoto kwa mamlaka kuleta ushahidi dhidi yake na akasema maafisa hawawezi kupata chochote muhimu.

Marekani kinyume na katiba iliweka watu milioni 1.5 kwenye orodha ya 'washukiwa', alisema.

Kitengo cha Usalama wa Rais kilimzuia Khairullah kuhudhuria dhifa ya Idul Fitr ya kila mwaka hata katika Ikulu ya White House, ambayo ni ukumbusho wa kumalizika kwa mwezi wa mfungo wa Waislamu wa Ramadhani.

Chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka mara tatu Marekani tokea hujuma za Septemba11 mwaka 2001 huku wanasiasa wakiitumia wakitumia chuki hiyo kuendeleza ajenda zao wenyewe, shirika la haki za kiraia la kutetea haki za Waislamu Marekani linasema.

Chuki dhidi ya Uislamu sasa inatekelezwa kwa njia iliyoratibiwa na kitaasisi nchini Marekani, Mratibu wa Utafiti na Utetezi katika Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR), Ammar Ansari, amesema.

3476971

Habari zinazohusiana
Kishikizo: cair marekani waislamu
captcha