Akizungumza katika hotuba ya televisheni Jumamosi jioni, Sheikh Naim Qassem aliapa kuendelea kupambana na Israel na akasema Hizbullah ina nguvu na uwezo wake ni mkubwa.
Alisema pia Lebanon ilikabiliwa na uchokozi wa kipekee, na Hizbullah ilisimama imara na kuipa Israel changamoto kubwa ya kijeshi.
Mahali pengine katika hotuba yake, mkuu huyo wa Hizbullah alimsifu kamanda wa zamani wa Iran dhidi ya ugaidi, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, akibainisha sifa zake za uongozi katika ngazi zote za kimkakati na kiakili.
Hafla aliyohutubia ilifanyika kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 5 ya shahidi huyu maarufu na mwenzake kutoka Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo Januari 2020.
"Shahidi Soleimani alikuwa kamanda mkuu wa Mhili wa Muqawama aliyevuruga njama za Marekani katika eneo la Asia Magharibi. Aliweza kurejesha hadhi ya suala la Palestina kupitia mapambano ya silaha katika maeneo yaliyokaliwa ya Palestina," alisema mkuu wa Hizbullah.
Alibainisha kuwa kamanda huyo wa zamani wa Iran dhidi ya ugaidi alifichua uovu wa Marekani na njama zake, hasa katika Iraq na Afghanistan.
Sheikh Qassem amesema Jenerali Soleimani alipambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIL au ISIS), na njama za Israel za kutawala eneo la Asia Magharibi.
Amesisitiza kuwa naibu mwenyekiti wa zamani wa Kitengo cha Uhamasishaji wa Umma cha Iraq (PMU), Abu Mahdi al-Muhandis, alikuwa na jukumu kubwa katika kuanzisha kikosi hicho kukabiliana na vikosi vya uvamizi vya Marekani na kusaidia Palestina.
3491327