Alizaliwa mwaka wa 1985, alijifunza usomaji wa Qur’an kutoka kwa kaka yake Reza Sharifi. Rahim ameshinda mara kadhaa katika mashindano ya Qur’ani ya Iran. Pia ni mwanachama wa kikundi cha Sabtayn Tawasheeh na ameshinda zawadi katika mashindano mbalimbali ya Tawasheeh. Raundi ya mwisho ya toleo la pili la Shindano la Kimataifa la Kisomo cha Qur’an la Al-Ameed ilizinduliwa Karbala na kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Qari kutoka nchi 22 wanashiriki katika tukio hilo la kimataifa la Qur’ani. Katika raundi ya kwanza, watu waliovutiwa waliwasilisha kipande cha video cha kisomo chao kwa kamati ya shindano na wale waliokuwa na utendaji bora walifika fainali.
Toleo la kwanza la Shindano la Kimataifa la Kisomo cha Qur’an la Al-Ameed katika Ramadhani yam waka jana lilivutia washiriki kutoka nchi 21. Linaandaliwa na Idara ya Mfawidhi wa Kaburi la Hadhrat Abbas (AS) kwa lengo la kukuza utamaduni wa Qur’ani.
3492166