Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree ametoa taarifa Jumanne asubuhi na kusema kwamba utawala vamizi wa Marekani unabeba dhima kamili ya kuleta vita katika Bahari ya Shamu na kushadidisha taharuki kwa kushambulia Yemeni.
Taarifa hiyo imesema: “Katika masaa machache yaliyopita, Vikosi vya Jeshi la Yemeni vimetekeleza kwa mafanikio shambulizi dhidi ya meli ya kivita ya Marekani yenye kusheheni ndege ya USS Harry Truman, katika kaskazini mwa Bahari ya Shamu kwa kutumia makombora mawili ya cruise na ndege mbili zisizo na rubani. Aidha tumeshambulia meli nyigine ya kivita ya Marekani kwa kombora moja la cruise na ndege nne zisizo na rubani."
Vikosi vya Jeshi la Yemeni vimeonya kwamba vitaendelea kushambua vikosi vyote vya adui katika Bahari ya Shamu na Bahari ya Arabu hadi mashambulio yao yamalizike.
Vikosi hivyo vinasisitiza kwamba havitaacha kushambulia malengo yote ya uadui katika Bahari ya Shamu na Bahari ya Arabu hadi mashambulio dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu yasimamishwe.
4272725
Jumamosi usiku, Marekani ilifanya mashambulio makubwa ya kivita dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sana’a, na majimbo kadhaa nchini humo, na kusababisha vifo na majeraha kwa watu wengi, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.
Ndege za kivita za Marekani na Uingereza zilifanya mashambulio 47 ya anga kwenye maeneo kadhaa katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a, pamoja na maeneo katika mkoa wa kaskazini wa Sa’ada, mkoa wa kati wa al-Bayda, na mkoa wa kusini-magharibi wa Dhamar.
Angalau watu 31, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, waliuawa katika mashambulio hayo ya anga na baharini yaliyoamriwa na Marekani.
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimewatumia salamu za kuwatakia amani wananchi wote adhimu wa Yemen na wale wote waliokomboka kifikra katika Umma wa Kiislamu ambao wametangaza upinzani wao dhidi ya uchokozi huo wa Marekani na kusisitiza kuwa, vitaendeleza operesheni zake za kuzuia meli za utawala wa Kizayuni zisipite katika eneo hadi pale mzingiro dhidi ya Ghaza utakapoondolewa.