IQNA

Maandamano ya mamilioni Yemen kwa ajili ya mshikamano na Wapalestina Gaza

8:18 - August 23, 2025
Habari ID: 3481124
IQNA – Watu wa Yemen katika mkoa wa Saada wameshiriki katika maandamano ya mamilioni ya watu Ijumaa, wakionesha mshikamano wao na watu wanaodhulumiwa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.

 

Maandamano hayo yalifanyika chini ya kauli mbiu: “Tunasimama pamoja na Gaza… Hatuyumbi kwa vitisho, wala hatuogopi njama.” 

Mwandishi wa Televisheni ya Al-Masirah aliripoti kuwa watu waumini wa Saada waliingia katika eneo la maandamano kwa makundi, wakijumuika katikati ya mji wa Saada.

Waandamanaji wa Kiyemeni walisisitiza tena msimamo wao wa dhati wa kuunga mkono wananchi wa Palestina na harakati zao za kupinga dhulma zinazoenezwa na utawala dhalimu wa Israel.

Kama ilivyokuwa kwenye maandamano yaliyopita, waandamanaji walionyesha uungaji mkono kamili kwa hatua za kujibu uhalifu wa utawala wa Kizayuni, na wakasisitiza utayari wao wa kukabiliana na uadui wa Marekani na Israel.

Watu wa Yemen wamekuwa wakitangaza waziwazi mshikamano wao na mapambano ya Palestina dhidi ya uvamizi wa Kizayuni, tangu utawala huo kuanzisha vita vya kikatili na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.

Vikosi vya Kijeshi vya Yemen tayari vimefanya mashambulio kadhaa dhidi ya malengo ya Israel kwa niaba ya watu wa Gaza. Wayemen wamesisitiza kuwa hawatasitisha mashambulizi dhidi ya Israel hadi mpaka mashambulizi ya utawala huo dhidi ya  Gaza yatakapositishwa. Tokea Oktoba 2023, utawala wa Kizayuni wa Israel umewaua Wapalestina wasiopungua 62,000 na kujeruhi wengine wengi zaidi. Aghalabu ya waathirika ni wanawake na watoto.

3494356

Habari zinazohusiana
Kishikizo: yemen gaza israel
captcha