Sayyid Abdul-Malik al-Houthi amesema bayana kwamba, kadiri utawala huo unavyoendelea na jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina huko Gaza, ndivyo Umma wa Kiislamu unavyozidi kuwajibika na kushadidi mashambulizi dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Kiongozi huyo wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kuwa, mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina yanatulazimisha kuzidisha operesheni zetu za kijeshi dhidi ya adui Mzayuni kwa kuzingatia uwajibikaji wetu wa kidini, kimaadili na kibinadamu.
Seyyed Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi ameongeza kuwa: "kadiri uchokozi wa utawala wa Kizayuni utakavyoenea na kurudiwa mara kwa mara, haijalishi na kamwe hilo halitaathiri nafasi ya watu wetu katika kuwaunga mkono wananchi wapendwa wa Palestina."
Kadhalika amesema, baada ya kusitishwa uchokozi wa Marekani kutokana na kushindwa kufikia malengo yake, utawala wa Kizayuni uko katika nafasi dhaifu na hivi sasa unajitahidi kujenga upya nafasi na hadhi yake iliyopotea kwa kukariri
mashambulio dhidi ya miundombinu ya raia wa Yemen.
Jeshi la Yemen limekuwa lilitekeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya ngome za utawala haramu wa Israel na kuusababishia utawala huo hasara kubwa za kijeshi na kiuchumi.
Opereshenei hizo za kishujaa za vikosi vya ulinzi vya Yemen zinafanywa kwa nia ya kuendelea kukabiliana na mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Yemen limesisitiza kuwa litaendeleza mashambulizi yake dhidi ya Israel hadi utawala huo utakapositisha jinai zake dhidi ya Wapalestina.
4285261