Kituo cha Masuala ya Qur’ani cha Shirika la Misaada na Wakfu nchini Iran kimetangaza kuwa taifa hilo litashiriki katika makundi mawili ya Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani Saudi Arabia.
Kulingana na kituo hicho: “Ndugu Mehdi Barandeh atashiriki katika kundi la kuhifadhi Qur’ani yote na Ndugu Seyed Hossein Moqaddam Sadat atawakilisha Iran katika kuhifadhi Juzuu 15 za Qur’ani Tukufu.”
Utaratibu wa kuchagua wawakilishi kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki mashindano ya kimataifa hufuata vigezo vya nchi mwenyeji na nafasi walizopata kwenye mashindano ya kitaifa. Mchakato huu unasimamiwa na Kituo cha Masuala ya Qur’ani cha Shirika la Wakfu na Misaada, pamoja na Kamati ya Kuwaalika na Kuwatuma Nje ya Nchi Wasomaji wa Qur’ani.
Tarehe rasmi ya mashindano haijatangazwa, lakini kwa kawaida hufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Safar (takribani Agosti), katika mji mtukufu wa Makka, karibu na Msikiti Mkuu.
Mwaka uliopita, Mohammad Hossein Behzadfar na Mohammad Mehdi Rezaei walishiriki katika makundi ya kuhifadhi Qur’ani yote na Juzuu 15 mtawalia.
Duniani, kuna mashindano matatu ya kimataifa yanayotajwa kuwa ya zamani zaidi: yale ya Malaysia ambayo hadi sasa yamefanyika mara duru 64, ya Saudi Arabia mara 44, na yale ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara 41.
3493704