Waandamanaji waliokuwa na wametuaja utawala wa Israel kuwa wa kikoloni kutokana na sera zake za kuendelea kupora ardhi za Wapalestina.
Maandamano hayo yameitishwa kufuatia tishio la hivi karibuni kutoka kwa maafisa wa utawala wa Israel kutaka kubadilisha Jiji la Gaza, ambalo lina wakaazi milioni moja wa Kipalestina, kuwa kifusi na kisha kupora ardhi hiyo.
Halikadhalika waandamanaji wameulaani vikali utawala wa Israel kwa kutumia njaa kama silaha dhidi ya Waplestina na hivyo wamesema dunia haipaswi kubaki kimya. Mapema wiki hii, Serikali ya Uingereza ilimwita balozi wa Israel Tzipi Hotovely, ambaye amekaa miezi 22 akijaribu kutetea vita vya mauaji kimbari vya Israel dhidi ya Gaza, kupinga upanuzi wa makazi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi. Kwa waandamanaji, hatua hiyo ya serikali ya Uingereza haina maana yoyote na wameitaja kuwa ya kimaonyesha tu kwa lengo la kutuliza hasira za umma. Waandamanaji walijitokeza na vyombo vya kupikia kama sufuria na vijiko kupiga kelele na kulaani matumizi ya Israel ya njaa kama silaha ya vita dhidi ya Wapalestina, huku polisi walijaribu kuwazuia bila mafanikio.
Halikadhalika waandamanaji wamesema msaada wa serikali ya Uingereza kwa utawala katili wa Israel unaifanya nchi hiyokuwa mshiriki katika mauaji wa kimbari. Waandamanaji pia walibeba mabango mbalimbali yenye kauli mbiu kama "Uhuru kwa Palestina," "Haki kwa Gaza," na "Njaa si silaha." Kwa kufanya hivyo, walionyesha msimamo wao si tu dhidi ya janga la kibinadamu bali pia dhidi ya sera za Israel.
Waandaji walisema maandamano haya yameonyesha kuwa umma wa Uingereza unafuatilia matukio yanayoendelea huko Gaza.
Pamoja na kuwa serikali ya Uingereza imekuwa ikiwapuuza waandamanaji wanaounga mkono Palestina na kulaani Israel, lakini waandamanaji wanasema wako tayari kuendelea kwa muda mrefu hadi haki ipatikane.. Tangu Oktoba 2023, vita vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza vimeua zaidi ya Wapalestina 62,300, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi ya 157,000.
3494363