IQNA

Morocco yaandaa Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mohammed VI

17:26 - August 28, 2025
Habari ID: 3481150
QNA – Toleo la 19 la Tuzo ya Kimataifa ya Mohammed VI ya Kuhifadhi, Kusoma, Tajweed, na Tafsiri ya Qur'ani lilifunguliwa Jumanne, Agosti 26, mjini Rabat, Morocco.

Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Morocco, Ahmed Toufiq, alitoa hotuba ya ufunguzi, akisisitiza kile alichokielezea kama uhusiano wa muda mrefu wa Wamorocco na Qur’ani. Alisema kwamba takribani nusu milioni ya wanafunzi, wakiwemo wanawake wengi, wanahudhuria shule za Qur’ani za kiasili kote nchini.

 Toufiq alielezea shukrani kwa wasomi wa Morocco na mchango wao katika kuhamasisha ujumbe wa Qur’ani kupitia "hoja sahihi na uchambuzi wa busara." Sherehe ya ufunguzi ilianza kwa usomaji wa Qur’ani kutoka kwa qari maarufu wa Morocco, Abdelkarim Al-Baqi Allah, akifuatiwa na hotuba kutoka kwa Abdelrahim Nablsi, ambaye ni mkuu wa jopo la majaji.

Pia ilionyeshwa video ikielezea kuhusu tuzo hii na kuonyesha taasisi zinazoongoza za Morocco zinazojitolea kukuza na kuhifadhi Qur’ani. Mashindano haya yanafanyika kila siku kuanzia saa 8 mchana hadi saa 2 usiku hadi Ijumaa. Yanawaleta pamoja wahifadhi Qur’ani, qari, na wasomi maarufu kutoka nchi za Kiarabu, Kiislamu, na Kiafrika, pamoja na washiriki kutoka Ulaya, Asia, na Morocco yenyewe.

3494405

captcha