IQNA

Hija na Umrah

Vifaa mahiri kuboresha viwango vya huduma katika Misikiti ya Makka na Madina

22:04 - January 20, 2025
Habari ID: 3480081
IQNA Vifaa mahiri vinatarajiwa kutumika kuboresha viwango vya huduma katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid Al Haram)  na Msikiti wa Mtume wa Medina (Al Masjid An Nabawi), afisa mmoja amesema.

Msikiti Mkuu wa Makka, mahali patakatifu zaidi katika Uislamu, una vyanzo 11 vikuu na vya ziada vya usambazaji wa umeme, na hakujawahi kuwa na haja ya kutumia mojawapo ya vituo vya nje vya ziada katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, afisa wa Saudia amesema.

Ghazi Al Shahrani, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka Kuu ya Huduma za Misikiti Miwili Mitakatifu, ameyasema hayo katika kikao cha hivi karibuni katika mji wa bandari wa Jeddah nchini Saudi Arabia kuhusu Hija na kuongeza kwamba Msikiti Mkuu ni wa kipekee ukilinganisha na maeneo mengine kwa sababu ni kituo kikubwa zaidi duniani, kinachofanya kazi zaidi kila wakati na mwaka mzima, na kinachotembelewa zaidi duniani.

"Hii inafanya suala la uendelevu kuwa la lazima na la hatima kwetu," afisa huyo aliongeza katika kikao kilichoitwa "Uendelevu na Ubora wa Vifaa na Huduma katika Misikiti Miwili Mitakatifu" kilichofanyika kama sehemu ya Mkutano na Maonyesho ya Hija wiki iliyopita.

Kwa mujibu wake, shirika la serikali linalosimamia misikiti miwili mitakatifu ya Uislamu kwa sasa linafanya kazi na washirika kupitisha programu za usimamizi kwa kutegemea vifaa mahiri na sensa za kisasa ili kuboresha viwango vya huduma.

Mamilioni ya Waislamu kutoka kote ulimwenguni hufika kila mwaka katika Msikiti Mkuu kutekeleza ibada ya kila mwaka ya Hija na Umrah.

Hajj, mojawapo ya majukumu ya lazima ya Kiislamu, inawataka Waislamu walio na uwezo wa kimwili na kifedha kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yao.

Takriban mahujaji milioni 1.8, wakiwemo milioni 1.6 kutoka nje, walitekeleza ibada za Hajj ndani na nje ya Mecca mwaka jana. Maandalizi yanaendelea kwa kasi kwa msimu ujao wa Hija.

/3491519

Kishikizo: umrah hija
captcha