Kwa mujibu wa tovuti ya qurancomplex.gov, kituo hicho kilipokea wageni 97,245 kutoka nchi 31 mwezi uliopita.
Miongoni mwao walikuwa mahujaji wa Umrah, wageni wa jiji la Medina, pamoja na washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdul Aziz.
Wageni hao, waliotoka nchi kama Indonesia, Ufaransa, Ujerumani, India, Pakistan, China, Iraq, Misri na Marekani, walipata fursa ya kufahamu hatua mbalimbali za uchapishaji na usambazaji wa Qur’ani Tukufu.
Ziara hizo zilifanyika kila siku, asubuhi na jioni, kwa mpangilio maalum wa kituo hicho.
Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd, kilichoanzishwa mwaka 1984 mjini Madina, kinajulikana sana kwa uzalishaji wake mkubwa wa nakala za Qur’ani Tukufu.
Ni kituo kikubwa zaidi duniani kinachojishughulisha na uchapishaji na usambazaji wa Qur’ani, kikizalisha takriban nakala milioni 10 kila mwaka, zikiwemo tafsiri na tarjuma kwa lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kiindonesia, Kirusi, Kijapani, Kiajemi, Kiurdu, Kibengali na Kikorea.
3494464