Sayyed Abbas Salehi, Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran ameyasema hayo siku ya Jumamosi katika mkutano wa kimataifa wa "Fikra za Nasrallah" na kuongeza: "Alikuwa ni mwanasiasa kamili kitaifa, kieneo na kimataifa na pia kamanda mkuu wa kijeshi wakati wa mashambulizi ya Israeli dhidi ya Lebanon."
Akifafanua zaidi kuhusu namna ambayo Shahidi Nasrallah alikuwa shakhsia wa kitaifa wa Lebanon na pia shakhsia wa Kiislamu wa kimataifa, Salehi alisema: "Ni nadra sana kwa mtu kuwa na sifa zote hizo."
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema: Shahidi Nasrallah alikuwa meneja wa kistratejia na meneja wa medani ya mapambano."
Aidha Salehi amesema kwamba Shahidi Nasrallah alijua vyema vyombo vya habari na diplomasia ya umma na alitumia vyema nyenzo hizo , na kuongeza kuwa : Njia ya Sayyed Hassan na njia ya Hizbullah bado ni imara na thabiti.
Kongamano la Kimataifa la Kuwaenzi Viongozi wa Muqawama lililopewa jina la 'Fikra ya Nasrallah' limefanyika jana mjini Tehran na kuhudhuriwa na wanazuoni kutoka nchi 13, zikiwemo Lebanon, Iraq, Bahrain, Misri, Kuwait, Uturuki, India, Malaysia, Algeria na Tunisia.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Iran, akiwemo Spika wa Bunge Mohammad Bagher Ghalibaf, Waziri wa Mambo ya Nje Seyed Abbas Araghchi, mkurugenzi wa Seminari za Kiislamu Ayatullah Ali Reza Aarafi na Ayatollah Mohsen Qomi, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kikao hicho cha siku moja kimelenga kutambulisha vipengele tofauti vya shakhsia na fikra za Shahidi Nasrallah na nafasi yake katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na mfumo wa kibeberu na kiistikbari duniani.
Sayed Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo la utawala wa kigaidi wa Israel kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.
3490614