IQNA

Muqawama

Tarehe ya mazishi ya Shahidi Nasrallah kutangazwa hivi karibuni

19:03 - November 27, 2024
Habari ID: 3479816
IQNA - Tarehe itatangazwa hivi karibuni kwa ajili ya mazishi ya marehemu kiongozi wa Hizbullah Shahidi Sayed Hassan Nasrallah, mbunge wa Lebanon alisema.

Ibrahim al-Musawi amesema hayo baada ya kutangazwa kusitishwa mapigano kati ya Hizbullah na utawala ghasibu wa Israel.

Ameyapongeza makundi yote ya Lebanon kwa makubaliano ya usitishaji vita na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kukubaliana nao baada ya kushindwa kufikia malengo uliyojiwekea kwa ajili ya vita dhidi ya Lebanon.

Utawala wa Israel ulijaribu kukandamiza harakati ya Hizbullah lakini ulishindwa kufanya hivyo na kulazimika kukubaliana na mapatano hayo, alisema.

Al-Musawi ameongeza kuwa mazungumzo juu ya usitishaji vita yalifanyika kwa njia isiyo ya moja kwa moja na kwamba Hizbullah inasisitiza kutekelezwa kwa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Aliendelea kusema kuwa kutatangazwa muda na mahali mwafaka kwa ajili ya mazishi ya kiongozi huyo aliyeuawa shahidi wa Hizbullah katika siku za usoni.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon yalianza kutekelezwa Jumatano alfajiri, na kuibua matumaini baada ya  miezi 14 ya vita.

Sayed Hassan Nasrallah, ambaye aliongoza Hizbullah kwa zaidi ya miaka 32, aliuawa shahidi katika shambulio kubwa la anga ambalo Israel ilitekeleza kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita ya Marekani.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa Hizbullah mwaka 1992 baada ya kuuawa kwa aliyekuwa katibu mkuu Abbas al-Musawi.

4250806

captcha