
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia tovuti ya Al-Mu’shir, matawi haya mapya yamefunguliwa kwa lengo la kuendeleza elimu ya dini na kuhifadhi Qur’ani Tukufu, sambamba na mafanikio ya jukwaa la kimataifa la kuhifadhi Qur’ani kwa njia ya mtandao.
Hatua hii inalenga kuwafikia wale wanaotamani kujifunza moja kwa moja katika maeneo ambayo hayakuwa na matawi ya taasisi hiyo.
Taasisi hiyo imeeleza kuwa lengo kuu ni kurahisisha mchakato wa kuhifadhi Qur’ani na kutoa fursa ya elimu ya dini kwa watu wa maeneo husika.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, uzinduzi wa matawi haya unatekelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikh Ahmed Al-Tayeb, Kiongozi Mkuu wa Al-Azhar, ambaye ameonyesha kujali sana maendeleo ya matawi ya Qur’ani ya Al-Azhar katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Abdul Munim Fouad, mmoja wa maafisa wa Al-Azhar, amesema kuwa ufunguzi wa matawi haya mapya ni daraja la kuziunganisha miji mipya na mtazamo wa wastani wa Al-Azhar.
“Tunalenga kutoa huduma bora za kielimu zisizo na fikra kali katika nyanja ya kuhifadhi Qur’ani na elimu zake, na kuwalinda vijana wetu na watoto dhidi ya misimamo mikali,” ameongeza.
Kwa upande wake, Hani Awdah, mfawidhi wa Msikiti wa Al-Azhar, amesema kuwa mchakato wa elimu katika matawi haya mapya utafuata viwango vya ubora na usahihi vinavyotumika katika Taasisi ya Kuhifadhi Qur’ani ya Msikiti Mkuu wa Al-Azhar.
Ameeleza kuwa ufunguzi wa matawi haya utatoa dirisha pana kwa maelfu ya watu wanaotamani kuhifadhi Qur’ani na kuelewa kwa undani elimu ya dini na ya kidunia.
4315907