IQNA

Mfalme wa Oman na viongozi wa nchi jirani wampongeza Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

18:04 - March 10, 2026
Habari ID: 3482037
IQNA – Sultani wa Oman amemtumia pongezi Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ujumbe alioutuma Jumatatu kwa Ayatullah Mojtaba Khamenei, Haitham bin Tariq alimtakia mafanikio katika kutekeleza majukumu yake mapya ya kuiongoza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akisisitiza uhusiano wa ujirani mwema kati ya Oman na Iran.

Ujumbe wa pongezi pia ulitumwa na viongozi wa nchi nyingine, wakiwemo mawaziri wakuu wa Iraq na Armenia pamoja na marais wa Turkmenistan na Jamhuri ya Azerbaijan.

Ayatullah Mojtaba Khamenei alichaguliwa Jumapili kumrithi marehemu baba yake, Imam Ayatullah Seyed Ali Khamenei, ambaye aliuawa shahidi katika shambulio la anga la kigaidi la Marekani na Israel lililolenga ofisi yake tarehe 28 Februari,siku ya kwanza ya mashambulizi ya kijeshi ya tawala hizo mbili za kigaidi dhidi ya Iran.

Katika kujibu mashambulizi hayo ya Marekani na Israel, ambayo pia yalisababisha kuuawa shahidi kwa makamanda kadhaa waandamizi wa kijeshi na mamia ya raia wakiwemo wanawake na watato,  Iran ilianzisha Operesheni ya kijeshi “Ahadi ya Kweli 4”, ambayo inajumuisha mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

3496702

Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha