IQNA

Bendera ya Rangi Tatu ya Muqawama (mapambano) yapeperushwa duniani

18:45 - April 01, 2026
Habari ID: 3482112
IQNA – Kadiri vita vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran vinavyoendelea, bendera ya rangi tatu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ishara ya wazi ya Muqawama au mapambano na ya iradaya pamoja ya wananchi, walioungana zaidi katika nyakati ngumu.

Haya yameelezwa katika makala ya Abbas Khameyar, aliyewahi kuwa mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Kuwait, Lebanon na Qatar. Makala yake inaeleza yafuatayo:

Katika siku hizi zenye misukosuko na katikati ya vita vilivyolazimishwa dhidi ya Iran, bendera ya Iran haipo tena kama alama rasmi pekee; imekuwa kama mpigo hai wa moyo wa taifa. Ni kana kwamba kila mtaa na kila kona, kila barabara na kila uwanja, umesimama kama simulizi hai, na bendera hizi za rangi tatu juu yake si kipande cha kitambaa kinachopeperuka tu hewani, bali ni dhihirisho la irada ya pamoja ya watu walioungana zaidi katika wakati mgumu.

Leo, bendera hii imeonekana kwa wingi usio wa kawaida mikononi mwa watoto na vijana, juu ya paa za nyumba, kwenye madirisha ya magari, na katika viwanja vya miji; uwepo unaotokana na hisia moja ya pamoja: kulinda utambulisho, ardhi, na haki ambayo watu huipa maana kwa maisha yao. Katika nyakati kama hizi, bendera haibaki tu alama ya nchi, bali huwa lugha ya moja kwa moja ya mshikamano na Muqawama—lugha inayowaunganisha watu wa makabila na mitazamo mbalimbali katika fremu moja.

Sauti ya uwepo huu sasa imevuka mipaka. Katika barabara za nchi za Kiislamu, za bara Afrika na pia za Magharibi kama vile Rome, London, Madrid, Paris na miji mingine mikuu ya dunia, na hata katika miji mbalimbali ya Marekani, bendera hii imepeperushwa; tukio ambalo kwa namna fulani linaonekana kuwa la kipekee katika historia ya nchi hizo. Ni kana kwamba alama ya taifa, katika mazingira ya mgogoro, imegeuka kuwa tamko la kimataifa linalogusa nyoyo katika sehemu mbalimbali za dunia.

Mandhari haya si matukio ya kupita tu; ni ishara kwamba katika nyakati za hatima, mataifa yanaweza kupata umoja kupitia majaribu, na kuibua umoja na sauti inayosikika duniani. Leo bendera ya Iran, katika wakati huu mgumu, haisimami tu juu ya ardhi, bali pia juu ya kilele cha maana na matumaini.

Kwa hitimisho, tunainamisha vichwa vyetu kwa heshima mbele ya bendera hii iliyoinuliwa na mbele ya wale wanaoibeba mabegani mwao katika giza la usiku, chini ya tishio la mabomu, wakiwa macho na thabiti.

Hao ni wabeba bendera wa kimya, waliodumisha roho ya kishujaa kwa subira na uthabiti wao.

Bendera hii, kwa heshima ya mikono yao, bado iko kileleni, na kilele hicho ni alama ya heshima na uthabiti wa taifa.

Flags of Iran

/3496948

Habari zinazohusiana
captcha