Wabunge 13 Waislamu wamechaguliwa katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini Uingereza na hivyo kuweka rekodi mpya iliyoongezeka kutoka wabunge 8 mwaka 2010.
Habari ID: 3276825 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/05/09
Licha ya duru za kimataifa kutoa onyo kali lakini mamlaka za Thailand zinaendelea kuwanyanyasa Waislamu ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku wanafunzi wa kike kuvaa vazi la staha la Hijabu.
Habari ID: 3217763 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/04/27
Viongozi wa dini mbalimbali wamehudhuria katika msikiti wa Tempe katika jimbo la Arizona nchini Marekani na kulaani vikali hatua ya kundi la kibaguzi na linalopiga vita Uislamu ya kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Habari ID: 3196196 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/04/23
Kiongozi wa ngazi ya juu wa Kiislamu nchini Ufaransa amesema kuwa misikiti 2200 nchini humo haiwatoshelezi mamilioni ya Waislamu wa Ufaransa na kutaka kuongezwa mara mbili idadi ya misikiti iliyopo katika muda wa miaka miwili.
Habari ID: 3099046 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/04/06
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ameahidi kuwa magaidi wa kundi la Kitakfiri la Boko Haram wataangamizwa katika kipindi cha mwezi moja ujao.
Habari ID: 3015828 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/20
Ripoti zinasema kuwa karibu miskiti yote 436 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imebomolewa kutokana na machafuko ya kidini.
Habari ID: 3008622 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/18
Umoja wa Mataifa umesema kuwa una wasiwasi kuhusu hali waliyo nayo Waislamu wa kabila la Rohingya wa huko Myanmar.
Habari ID: 3001295 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/17
Mjumbe katika Baraza la Kaunti ya mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya amekosoa uamuzi wa Mahakama Kuu kuwapiga marufuku wanafunzi Waislamu katika Kaunti ya Isiolo kuvaa Hijabu.
Habari ID: 2968360 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/12
Wanafunzi Waislamu katika jiji la New York wamekuwa wakikabiliwa na miamala ya kibaguzi na kuvunjiwa heshima kutokana na kuongezeka hisia za chuki dhidi ya dini Tukufu ya Uislamu nchini Marekani.
Habari ID: 2954393 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/09
Rais John Mahama wa Ghana amesema wanawake Waislamu nchini humo wana haki ya kuvaa vazi la Hijabu.
Habari ID: 2930968 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/05
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatekeleza mkakati wa kuhakikisha inageuka na kuwa kitovu cha utalii halali kwa lengo la kuwavutia Waislamu milioni 15 kutoka maeneo mbali mbali duniani.
Habari ID: 2910925 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/28
Waislamu nchini Marekani wameelezea wasi wasi wao kutokana na kuongezeka wimbi la ubaguzi na hujuma dhidi yao.
Habari ID: 2897132 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/25
Waislamu nchini Cuba wametoa wito wa kujengwa msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo, Havana.
Habari ID: 2877957 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/21
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa: “Taifa la Iran daima limeonesha kuwa lina irada imara na lina uwezo na kuvunja njama za adui.”
Habari ID: 2869495 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/19
Kuuliwa vijana watatu wanachuo Waislamu katika jimbo la Carolina Kaskazini nchini Marekani ni kitendo kinachopaswa kulaaniwa na ni kiashiria kingine cha hatari kubwa ya kuenea kwa vitendo vya ukatili na uchupaji mipaka.
Habari ID: 2858484 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/16
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza katika taarifa yake kuwa Waislamu watatu waliouawa hivi karibuni mjini Chapel Hill nchini Marekani walikuwa wakishiriki kwenye shughuli za utoaji misaada ya kibinadamu na ni wawakilishi wa thamani bora za uraia wa ulimwengu mzima.
Habari ID: 2851644 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/15
Serikali ya Myanmar imetangaza kuwa, Waislamu wa kabila la Rohingya hawana haki ya kupiga kura katika kura ya maoni ya katiba ya nchi hiyo.
Habari ID: 2846218 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/13
Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi ya wanachuo watatu Waislamu ambao waliuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Chapel Hill jimbo la Carolina Kaskazini.
Habari ID: 2846215 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/13
Kuongezeka vitendo vya ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa kumeendelea kulaaniwa na kukosolewa na jamii ya Waislamu sio tu nchini humo bali pia katika bara zima la Ulaya.
Habari ID: 2829282 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/09
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kujiepusha na ugaidi, misimamo mikali na utumiaji mabavu kwa kisingizio cha kulinda dini.
Habari ID: 2743220 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/22