iqna

IQNA

Maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran Jumatatu wameandamana mbele ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kulaani hatua ya gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa ya kuchapishwa tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW).
Habari ID: 2736722    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/20

Katika mwendelezo wa chuki dhidi ya dini na matukufu ya Kiislamu, Marekani imepiga marufuku adhana katika Chuo Kikuu cha Duke nchini humo.
Habari ID: 2736720    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/20

Waislamu wa kila pembe duniani wameendelea kulaani vikali kitendo cha jarida linalochapishwa Ufaransa la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena picha za vikatuni vya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 2720426    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/18

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Markel amesema kuwa, Waislamu wanaoishi nchini humo ni .miongoni mwa jamii ya Wajerumani
Habari ID: 2706291    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/13

Stephen Le Foll, Msemaji wa serikali ya Ufaransa ametembelea na kukagua msikiti ulioko katika eneo la Port- la- Nouvelle kusini mwa nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, msikiti huo ulishambuliwa kwa maguruneti matatu.
Habari ID: 2700801    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/12

Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na makundi ya kigaidi na kitakfiri, ninamtukanisha Mtume Muhammad SAW, Qur'ani na umma wa Kiislamu.
Habari ID: 2692014    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/10

Waliul Amr wa Waislamu kote duniani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, umoja ni somo kubwa kutoka kwa Mtume wa Mwisho SAW na kwamba hivi sasa ni hitajio la dharura la umma wa Kiislamu.
Habari ID: 2689577    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/09

Hivi sasa tumo katika Wiki ya Umoja kati ya Waislamu ambayo ilitangazwa na hayati Imam Khomeini kutokana na hitilafu za mapokezi kuhusu siku aliyozaliwa Mtume Muhammad SAW. Wiki hiyo inaanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal.
Habari ID: 2684362    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/08

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kibeberu yanaibua migogoro baina ya Waislamu kwa lengo la kutawala ardhi za Kiislamu zenye umuhimu wa kistratijia.
Habari ID: 2684305    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

Katibu Mkuu wa OIC
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amesema kuwa, Waislamu wote wana haki ya kuingia katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.
Habari ID: 2677828    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/06

Kiongozi wa Harakati ya al-Huthi nchini Yemen, ametaka kulindwa umoja kati ya makundi ya kisiasa na kuwepo makubaliano na mshikamano wa kitaifa katika kukabiliana na njama za kigeni kwa ajili ya kutoa pigo kwa umoja nchini Yemen.
Habari ID: 2672152    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/05

Mwenyekiti wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran amesema lengo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu ni kuimarisha itikadi za wanafunzi wa vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu ili kuhuisha umoja wa Waislamu kueneza ustaarabu mpya wa Kiislamu.
Habari ID: 2666237    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/01

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio linaloitaka serikali ya Myanmar kuwapa haki kamili ya uraia Waislamu wa Rohingya.
Habari ID: 2663155    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/01

Kiongozi mwandamizi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Uganda Sheikh Ductoor Abdul Qadir Sudi Muwaya aliuawa shahidi Alkhamisi iliyopita. Mkuu wa polisi nchini humo ametangaza kuwa uchunguzi wa kina utafanyika kubainisha aliyetekeleza mauaji hayo.
Habari ID: 2646978    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/29

Mamia ya Waislamu nchini Sweden waliandamana Ijumaa kulaani kitendo cha kushambuliwa msikiti mmoja kwa bomu la petroli siku ya Alkhamisi.
Habari ID: 2637292    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/27

Kutokana na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu huko Malawi, Waislamu nchini humo wameanzisha kampeni ya kuwashawishi wafuasi wa dini nyinginezo kuzingatia msingi wa ‘kuishi pamoja kwa amani’ ili kuzuia uwezekano wa kuibuka malumbano ya kidini katika nchi hiyo ya kusini wa Afrika.
Habari ID: 2621819    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/18

Waislamu nchini Kenya wanataka vyombo vya habari nchini humo vifanye mabadiliko ya kimsingi kuhusu namna vinavyo tangaza habari kuhusu ugaidi na kuonya kuwa mfumo wa sasa usio wa kitaalamu wa kutangaza habari ni chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Habari ID: 2617613    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/11

Wafanya magendo ya binadamu wanawatumia vibaya wakimbizi Waislamu wanaokimbia mauaji na unyanyasaji wa kuchupa mipaka nchini Myanmar.
Habari ID: 2613658    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/01

Imam Khamenei
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumanne mjini Tehran ameonana na maulamaa, wanavyuoni, wasomi na wageni walioshiriki kwenye Kongamano la Kimataifa la Mirengo ya Kitakfiri kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu na kulitaja suala la kuzuka upya makundi ya kitakfiri katika miaka ya hivi karibuni kuwa ni tatizo lililopandikizwa na mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2612034    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/26

Waislamu nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali ya nchi hiyo kufunga misikiti kadhaa katika Kaunti ya Mombasa.
Habari ID: 1476305    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/23