waislamu - Ukurasa 95

IQNA

Wizara ya Elimu na Masuala ya Kidini Ugiriki imetangaza kuwa Waislamu mjini Athens watatengewa nafasi maalumu kwa ajili ya Sala ya Idul Fitr, ambayo husaliwa baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3470370   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/08

Serikali ya China, kwa mara nyingine, imewaamuru wanafunzi, wafanya kazi wa umma na hata wakaazi wa kawaida katika eneo lenye Waislamu wengi la Xinjiang kutofunga Saum ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3470369   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/08

Waislamu nchini Marekani katika jimbo la New Mexico wametangaza kuimarisha harakati za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Habari ID: 3470364   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/07

Baadhi ya nchi za Kiarabu zimetangaza tarehe 6 Juni kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3470361   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/06/06

Chuki dhidi ya Uislamu
Kundi la wanaume jimboni Texas nchini Marekani wanapata mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwaua Waislamu huku wakitumbukiza risasi zao katika damu au mafuta ya nguruwe katika mazoezi hayo.
Habari ID: 3470345   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/29

Sheikh Ahmad Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri amesema chuo hicho kitaanzisha televisheni ya satalaiti itakayorusha matangazo kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa ili kuwasilisha taswira sahihi ya Uislamu katika nchi za Magharibi.
Habari ID: 3470343   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/29

Kiongozi wa Kikristo nchini Samoa ameitaka serikali ya nchi hiyo ya Bahari ya Pasifiki kuupiga marufuku Uislamu.
Habari ID: 3470335   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/25

Waislamu wa Marekani hawakabiliwi na matatizo katika kipindi cha uhai wao tu bali hata wanapofariki dunia matatizo hayo bado huwaandama.
Habari ID: 3470331   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/24

Kikao cha kila mwaka wachaposhaji Qur'ani Tukufu barani Afrika kinaanza Alkhamisi hii nchini Sudan.
Habari ID: 3470321   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/19

Shirika moja la kutoa misaada nchini Uingereza limeanzisha kampeni ya matangazo yenye mabango ya 'Subhan Allah' kwa ajili ya kushajiisha watu watoe misaada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3470304   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/10

Mikutano wa "Wanafunzi Waislamu, Dunia Isiyo na Machafuko" na mwingine wa "Nafasi ya Wasomi wa Utamaduni Katika Ulimwengu wa Kiislamu ili Kufikia Dunia Isiyo na Machafuko" imepangwa kufanyika wiki ijayo nchini Senegal.
Habari ID: 3470292   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/04

Mwanachama mwandamizi wa chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema serikali inataka kurekodi na kufanya ujasusi kuhusu hotuba katika misikiti nchini humo.
Habari ID: 3470284   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/02

Mahakama ya Nigeria imeunda tuma ya uchunguzi kuhusu mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu Desemba 2015.
Habari ID: 3470280   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/05/01

Serikali ya Uswisi imesitisha mchakato wa kuzipa uraia familia mbili za Waislamu ambao watoto wao wawili wa kiume mabarobaro walikataa kuwapa mikono walimu wao wa kike.
Habari ID: 3470257   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/20

Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Kampala amekutana na Mufti Mkuu wa Uganda na kujadilia njia za kushirikiana nchi mbili katika harakati za Qur'ani.
Habari ID: 3470252   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/18

Serikali ya Nigeria imekiri kuwazika Waislamu 347 wa madhehebu ya Shia katika kaburi la umati mwezi Desemba mwaka 2015.
Habari ID: 3470245   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/13

Mwanafunzi wa zamani wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, amebainisha wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya ya mwanazuoni huyo.
Habari ID: 3470243   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/12

Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema Waislamu ni waathirika wakuu wa ugaidi duniani.
Habari ID: 3470236   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/09

Viongozi wa utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia wamepiga marufuku kutangazwa adhana katika misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mkoa wa Al-Hasa, mashariki mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3470222   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/01

Waislamu nchini Marekani wanakabiliana na wimbi jipya la chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia hata baada ya kuwa wamelaani vikali hujuma ya kigaidi mjini Brussels, Ubelgiji Jumanne hii.
Habari ID: 3470215   Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/26