waislamu - Ukurasa 97

IQNA

Takribani miaka 1376 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW Imam Hussein bin Ali AS akiwa na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.
Habari ID: 3459320   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/12/02

Kundi la kigaidi Boko Haram limetangaza kuhusika na shambulio dhidi ya msafara wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia waliokuwa katika msafara wa maombolezo ya Imam Hussein AS jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
Habari ID: 3458202   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/29

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali nchini Kenya kuzidisha ushirikiano na urafiki miongoni mwao ili kuepusha fitina za kidini na kimadhehebu.
Habari ID: 3457358   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/26

Vitendo vya chuki na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa vinaripotiwa kuongezeka siku baada ya siku hasa baada ya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris.
Habari ID: 3455375   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/22

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini Ufaransa imethibitisha kuwa gaidi aliyepanga na kuratibu mashambulizi ya kigaidi ya Paris ameuawa.
Habari ID: 3454889   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/21

Kamati ya haki za binadamu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya Myanmar iheshimu haki za jamii ya Waislamu wa Rohingya walio wachache katika nchi hiyo.
Habari ID: 3454884   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/21

Warsha ya kuhusu kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS imefanyika Bauchi nchini Nigeria.
Habari ID: 3454535   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/19

Misikiti 10 mipya inatazamiwa kujengwa nchini Mali magharibi mwa Afrika kupitia ufadhili wa Taasisi ya Misaada ya RAF.
Habari ID: 3454532   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/19

Qur’ani Tukufu inawaita watu wote kuelekea katika akili, hekima na mazungumzo ya kimantiki, amesema mwanazuoni mwandamizi nchini Iran.
Habari ID: 3443991   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/06

Wanafunzi Waislamu wanaosoma katika shule za umma au za binafsi zisizokuwa za Waislamu katika jimbo la California nchini Marekani wamefanyiwa uonevu au ubaguzi kwa kiwango cha zaidi ya mara mbili kwa wastani wa kitaifa.
Habari ID: 3432361   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/02

Aplikesheni za kusoma Qur’ani Tukufu zinaendelea kupata umashuhuri katika nchi za Kiislamu na hata nchi zisizokuwa za Kiislamu kote duniani.
Habari ID: 3428150   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/11/01

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa Myanmar itakumbwa na mgogoro mkubwa iwapo uchaguzi wa wiki ijayo hautazingatia vigezo muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapa Waislamu haki ya kupiga kura.
Habari ID: 3421779   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/31

Kiongozi wa Ansarullah
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema watawala madhalimu wanapanga njama za kudhoofisha umma wa Kiislamu kwa kuuweka mbali na thamani za misingi ya haki.
Habari ID: 3393529   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/25

Jeshi la Israel limewaua shahidi Wapalestina wapatao 46 tangu kuanza Intifadha au mwamko mpya mapema mwezi huu wa Oktoba.
Habari ID: 3390450   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/19

Rais Vladimir Putin wa Russia ameidhinisha muswada wa bunge la nchi hiyo, Duma, kuhusu kulinda na kuhifadhi heshima vitabu vitukufu vya duni kubwa duniani.
Habari ID: 3386346   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/17

Umoja wa Wanawake Waislamu Duniani wametoa taarifa ya rambirambi kufuatia kuuawa maelfu ya mahujaji kutoka nchi mbali mbali katika mkanyangano wa Mina karibu na mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3385195   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/13

Ayatollah Araki
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimatiafa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Ayatollah Mohsen Araki ametoa wito kwa wanazuoni wa Kiislamu kufuatilia suala la kuundwa Umoja wa Nchi za Kiislamu.
Habari ID: 3384011   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/11

Misikiti Marekani imetakiwa kuwa katika hali ya tahadhari na kuimarishwa usalama kutokana na ghasia zinazotazamiwa kuibuliwa Oktoba 10 na makundi ya watu wenye misimamo mikali ya chuki dhidi ya Uislamu ambao wataandamana siku hiyo.
Habari ID: 3382994   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/07

Rais Vladmir Putin wa Russia Jumatano amefungua msikiti mkuu wa Moscow ambao ni msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya.
Habari ID: 3366927   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/24

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Hija katika mwaka 1436 Hijria. Ifuatayo ni matini kamili ya ujumbe huo
Habari ID: 3366752   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/23