iqna

IQNA

mtume muhammad saw
TEHRAN (IQNA) - Wimbi kali la maandamano ya kulaani matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akitetea matusi na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW Nchini humo limeendelea kushuhudiwa katika pembe mbalimbali za dunia.
Habari ID: 3473325    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe marais wa nchi za Kiislamu akiwapongeza kwa mnasaba wa kuadhimisha Maulidi na siku ya kuzaliwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na Nabii wa rehma, upendo na amani, Muhammad SAW.
Habari ID: 3473324    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Hotuba ya Miladj un Nabii SAW
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia siasa za kimantiki za kusimama kidete kukabiiliana na sera za kibabe za Marekani na kusema kuwa, sera zenye mahesabu za Jamhuri ya Kiislamu hazibadiliki kwa kuondoka kiongozi na kuja mwingine madarakani huko Marekani.
Habari ID: 3473323    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

Mwanazuoni wa Lebanon
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Lebanon amesema umoja wa Waisalu ni sera bora zaidi katika kukabiliana na maadui wanaouhujumu Uislamu na kuvunjia heshima matukufu yake.
Habari ID: 3473320    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/02

TEHRAN (IQNA) - Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameonekana kuanza kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya Waislamu na sasa amelegeza msimamo wake mkali wa awali wa matamshi yaliyojaa chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3473319    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/02

TEHRAN (IQNA)- Rais Joko Widodo wa Indonesia amelaani kauli ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa dhidi ya Uislamu na kusema mtawala huyo amewatusi Waislamu wote duniani.
Habari ID: 3473316    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/01

TEHRAN (IQNA)- Mfunguo Sita Rabiul Awwal ni mwezi ambao Waislamu kote duniani wanashereheka siku aliyozaliwa Mtume Muhammad SAW, siku ambayo ni maarufu kama Maulidi.
Habari ID: 3473314    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/31

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amelaani hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi Ufaransa na wakati huo huo pia amelaani matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu ya Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo.
Habari ID: 3473313    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/31

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kitendo chochote cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW maana yake ni kuwavunjia heshima Mitume wote na vitabu vya mbinguni.
Habari ID: 3473311    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/30

Wiki ya Umoja wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Mkutano wa 34 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza kufanyika mjini Tehran ukihudhuriwa na shakhsia 167 wa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3473310    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/30

Kiongozi wa Ansarullah
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema rais Emmanuel Macron wa Ufaranmsa ni kikaragosi kinachochezeshwa na Wazayuni kichukue hatua za kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu.
Habari ID: 3473309    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/30

Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kama nchi za Magharibi, za Ulaya na Ufaransa ni wakweli katika madai yao kwamba zinapigania amani, udugu, usalama na utulivu katika jamii ya mwanadamu basi zinapaswa kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Waislamu.
Habari ID: 3473307    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/29

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwahutubu vijana Wafaransa
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kushangazwa kwake na undumakuwili wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kulikingia kifua jarida la Charlie Hebdo la nchini hiyo ya Ulaya kwa kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.
Habari ID: 3473306    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/29

TEHRAN (IQNA)- Baada ya kuchapishwa katuni zinazommvunjia heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa na baada ya hapo matamshi ya Rais Macron wa nchi hiyo kutoa matamshi yenye chuki dhidi ya Uislamu, Waislamu kote duniani wameandamana kulaani vitendo hivyo huku wakiitaka bidhaa za Ufaransa zisusiwe.
Habari ID: 3473305    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/28

TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja katika wilaya ya Vernon kaskazini mwa Ufaransa umepokea vitisho vya kushambuliwa huku chuki dhidi ya Uislamu ikishadidi nchini humo.
Habari ID: 3473304    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/28

TEHRAN (IQNA- Balozi Mdogo wa Ufaransa mjini Tehran, Florent Aydalot, ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kukabidhiwa malalamiko ya Iran kuhusu sisitizo la serikali ya Ufanrasa la kuwaunga mkono waliochapisha katuni zilizomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473299    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/27

TEHRAN (IQNA) -Malalamiko na ukosoaji dhidi ya matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akitetea vitendo vya kutusiwa na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW nchini humo unaendelea kupamba moto huku nchi mbalimbali za Kiislamu zikitoa wito wa kuiadhibu Paris kwa kususia bidhaa za Ufaransa.
Habari ID: 3473297    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/26

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema nuru ya Mtume Mtukufu wa Uislamu, SAW, haiwezi kuzimwa kwa njama za maadui wa Kiislamu na kwamba njama hizo zitarejea kuwadhuru wao wenyewe.
Habari ID: 3473296    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/26

TEHRAN (IQNA) - Makundi ya kupigania ukombozi Palestina yamemlaani Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutokana na hatua yake ya kuunga mkono michoro ya kikatuni yenye kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473295    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/25

TEHRAN (IQNA) – Wanawake wawili ambao waliwashambuliwa wanawake wengine Waislamu waliokuwa wamevaa Hijabu mjini Paris, wamefikishwa kizimbani.
Habari ID: 3473289    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/23