iqna

IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /24
TEHRAN (IQNA) – Shaban Abdul Aziz Sayyad alikuwa miongoni mwa makari mashuhuri wa Misri ambaye alisoma Qur’ani kwa shauku na usomaji wake ulikuwa maarufu sana.
Habari ID: 3476482    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/29

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Wakfu wa Misri amesema wawakilishi wa nchi 58 watashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya nchi hiyo.
Habari ID: 3476481    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/29

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) - Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) imelaani vikali vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya, na kubainisha kwamba vitendo hivyo viovu vinaonyesha "chuki kubwa" ya maadui dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3476479    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/28

Harakati za Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Sherehe ilifanyika katika Mkoa wa Tokat, kaskazini mwa Uturuki, kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi 258 ambao wameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3476478    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/28

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ilitangaza uzinduzi wa usajili kwa ajili ya mashindano ya 13 ya Qur'ani Tukufu nchini humo.
Habari ID: 3476477    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/28

Iran ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Baada ya kuswali Sala ya Ijumaa, wananchi kote katikaa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamejitokeza mitaani na kulaani hatua za hivi karibuni za nchi za Magharibi na Ulaya zikiongozwa na Marekani za kudhalilisha matukufu ya Kiislamu na kuliwekea vikwazo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Habari ID: 3476471    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/27

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema serikali za Magharibi zinaunga mkono kuvunjiwa heshima dini za Mwenyezi Mungu hususan Uislamu.
Habari ID: 3476470    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/27

Chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Iran amekashifu kudharauliwa kwa Qur'ani Tukufu na kusema ni dharau kwa Dini za Abrahamu (Ibrahimu )
Habari ID: 3476468    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/26

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini wa Bahrain Sheikh Isa Qassim amelaani vikali kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu hivi karibuni katika nchi za Ulaya.
Habari ID: 3476466    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/26

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa taarifa kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi kadhaa za Ulaya na kusisitiza kuwa: "Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kiwendawazimu chini ya nara ya 'uhuru wa maoni' ni ishara kuwa uistikbari unalenga Uislamu na Qur'ani Tukufu."
Habari ID: 3476465    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/26

Kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu Ulaya
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimetoa wito wa kususia bidhaa za Uswidi na Uholanzi ili kukabiliana vitendo viovu vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika mataifa hayo ya Ulaya hivi karibuni.
Habari ID: 3476461    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/25

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /21
TEHRAN (IQNA) – Abdel Aziz Akasha alikuwa qari wa Misri ambaye alipata umaarufu baada ya kuanzisha mtindo maalum katika usomaji wa Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3476457    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/24

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Baada ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Uswidi mwishoni mwa juma, kulikuwa na kitendo kingine cha kufuru kilichotekelezwa na mmoja wa vinara wa harakati za chuki dhidi ya Uislamu Ulaya, wakati huu nchini Uholanzi.
Habari ID: 3476456    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/24

Mashindano ya Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Washindi wa toleo la 23 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum la Falme za Kiarabu katika kitengo cha wanaume wametunikiwa zawadi.
Habari ID: 3476455    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/24

Taazia
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu Mauritania ambaye amenadika tarjuma ya Qur’ani Tukufu Mohamed Mokhtar Ould Abah amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Habari ID: 3476454    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/24

Shakhsia Katika Qur'ani Tukufu / 28
TEHRAN (IQNA)- Isipokuwa Bibi Maryam, hakuna mwanamke mwingine ambaye ametajwa moja kwa moja katika Quran Tukufu. Lakini kuna majina yasiyo ya moja kwa moja ya wanawake Waumini na makafiri.
Habari ID: 3476453    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/23

Harakati za Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Taasisi ya kutoa misaada ya Uturuki ilitoa zaidi ya nakala 11,000 za Misahafu (Qur'ani Tukufu) kwa Waislamu katika nchi tofauti za Kiafrika mwaka jana.
Habari ID: 3476451    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/23

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imejiunga nan chi za Kiislamu duniani kulaani kitendo cha hivi punde zaidi cha kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Sweden (Uswidi), na kusisitiza kuwa kuudhi matukufu ya Umma wa Kiislamu ni jambo lisilokubalika.
Habari ID: 3476448    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/22

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejiunga na ulimwengu wa Kiislamu katika kulaani vikali kitendo cha kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Sweden (Usiwidi).
Habari ID: 3476444    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/22

Harakati za Qur'ani Kimataifa
TEHRAN (IQNA) - Mwambata wa kitamaduni wa Iraq nchini Malaysia alisema Tamasha la Sanaa la Qur'ani la Kimataifa la Restu linawapa watu fursa ya kujifunza kuhusu kazi za kimataifa za sanaa ya Qur'ani.
Habari ID: 3476441    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/21