mashindano ya qurani - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Chuo Kikuu cha Al-Ameed kimeandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an yanayojulikana kama “Qur'an Al-Nur”, yakihusisha wanafunzi kutoka zaidi ya vyuo vikuu 60 vya ndani na nje ya Iraq.
Habari ID: 3481375    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 26 ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind bint Maktoum imeanza rasmi Dubai, ikiwakutanisha wanaume na wanawake wanaohifadhi Qur’ani kutoka kote katika Muungano wa Falme za Kiarabu.
Habari ID: 3481372    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15

IQNA-Idara Kuu ya Mambo ya Kiislamu, Awqaf na Zakat ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imetangaza kuanza kwa usajili wa toleo la pili la Emirates International Quran Award.
Habari ID: 3481367    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/14

IQNA – Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yatafanyika wakati wa toleo la pili la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Libya, yatakayofanyika mjini Tripoli mwishoni mwa mwezi huu.
Habari ID: 3481363    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, yakihusisha washiriki 330 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, yatafanyika mwaka huu katika mji wa Sanandaj ulioko magharibi mwa Iran, chini ya kauli mbiu: “Qur'ani, Kitabu cha Umoja.”
Habari ID: 3481362    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13

IQNA – Mtaalamu mkongwe wa Qur'an, Abbas Salimi, amesema kuwa mashindano ya Qur'an yana mchango mkubwa katika kuimarisha jamii na kuzuia Qur'an Tukufu kusahaulika au kuwekwa pembeni.
Habari ID: 3481352    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/11

IQNA – Qari maarufu wa Iraq na mtangazaji wa televisheni Sayyid Hassanayn al-Hulw ameisifu mashindano mapya ya Qur’an ya Iran yaliyopewa jina la “Zayin al-Aswat”, akiyataja kuwa jukwaa la mabadiliko linalofichua vipaji vya kipekee vya vijana na kuimarisha misingi ya elimu ya Qur’an.
Habari ID: 3481340    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/08

IQNA – Mashindano ya Qur'an kama ‘Zayin al-Aswat’ huwapa vijana msukumo wa kiroho na hutoa kipimo sahihi cha maendeleo yao katika usomaji wa Qur'an, amesema Qari maarufu kutoka Iran, Ahmad Abolqassemi.
Habari ID: 3481337    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/07

IQNA – Profesa Abdul Karim Saleh, Mkuu wa Kamati ya Mapitio ya Qur’ani ya Al-Azhar, ametangazwa na kupewa heshima kama “Mtu wa Mwaka wa Qur’ani” katika Tuzo ya 13 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Libya.
Habari ID: 3481331    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/05

IQNA – Qari kijana kutoka Iran aliyeshiriki katika toleo la kwanza la mashindano ya Qur’ani ya ‘Zayin al-Aswat’(mapambo ya sauti) amesifu ubora wa mashindano hayo na kuyataja kuwa fursa muhimu ya kutambulisha wasomaji wa Qur’ani wasiojulikana sana nchini.
Habari ID: 3481323    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/03

IQNA – Hafla ya kufunga mashindano ya kwanza ya kitaifa ya Qur’ani yenye jina “Zayen al-Aswat” (mapambo ya sauti) ilifanyika siku ya Alhamisi mjini Qom, ambapo washiriki bora walienziwa na kutunukiwa zawadi.
Habari ID: 3481322    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/03

IQNA – Mkurugenzi mtendaji wa toleo la kwanza la mashindano ya Qur'ani ya kitaifa ya ‘Zayin al-Aswat’ (mapambo ya sauti) amesema kuwa katika mashindano mengi ya Qur'an, kila kitu huisha kwa sherehe ya kufunga na kuwatuza washindi na sasa sekretarieti ya tukio hili la Qur'an inalenga kuandamana na washiriki kupitia mawasiliano endelevu na yenye tija ili kuwafikisha katika viwango vya kitaalamu na vya kimataifa.
Habari ID: 3481314    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/01

IQNA – Ahmad Abolqassemi, Qari mashuhuri kutoka Iran, amesisitiza uwezo wa kipekee wa nchi hiyo katika uwanja wa usomaji wa Qur’ani Tukufu, akipendekeza kuandaliwa mashindano mapya ya kipekee ya “fainali ya mabingwa” kwa washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, yatakayofanyika nchini Iran.
Habari ID: 3481300    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29

IQNA – Libya imetangaza washindi wa Tuzo ya 13 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu, iliyofikia tamati mjini Benghazi kwa ushiriki wa zaidi ya mataifa 70.
Habari ID: 3481299    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29

IQNA – Toleo la kwanza la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya Iran ya “Zayin al-Aswat” (mapambo ya sauti) linatarajiwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Qom, likijumuisha makundi matatu kuu, waandaaji walitangaza.
Habari ID: 3481298    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/28

IQNA-Mashindano ya sita ya kuhifadhi, kusoma, na Tajwidi ya Qur’ani Tukufu nchini Morocco yameingia katika hatua ya mwisho, yakifanyika kuanzia Ijumaa katika mji wa Fez.
Habari ID: 3481290    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/27

IQNA – Majina ya wale wanaostahiki kushiriki katika hatua ya fainali ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran yametangazwa.
Habari ID: 3481277    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/24

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya Mfalme Salman bin Abdulaziz ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume (SAW) barani Afrika imehitimishwa kwa hafla rasmi iliyofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Habari ID: 3481271    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/23

IQNA – Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 39 ya Kitaifa ya Qur’ani na Etrat kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Iran imepangwa kufanyika katika mji wa kati wa Isfahan.
Habari ID: 3481268    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/22

IQNA – Mji wa Benghazi ulioko kaskazini mashariki mwa Libya ni mwenyeji wa toleo la 13 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya nchi hiyo.
Habari ID: 3481261    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21