iqna

IQNA

Mwanaharakati wa Qur'ani kutoka nchini Iraq ameashiria Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu na kusema mashindano hayo ni fursa muafaka kwa washiriki kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 2663153    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/01

Baada ya kutoa mafunzo kwa Maimamu wa miskiti kutoka nchi kadhaa za Afrika, Morocco sasa imesema itatoa mafunzo kwa maimamu 50 kutoka Ufaransa.
Habari ID: 2625018    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/22

Takribani watu milioni 20 wamewasili Karbala kwa ajili ya kushiriki katika Arubaini ya Imam Husain AS. Mkuu huyo wa mkoa wa Karbala amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kabisa kumiminika watu kiasi chote hicho katika historia ya ziara za Imam Husain AS.
Habari ID: 2617895    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/13

Waziri wa Ulinzi wa Iraq amesema kuwa, wafanyaziara milioni 17.5 wamekusanyika katika mji mtukufu wa Karbala kwa ajili ya kushiriki maombolezo ya siku ya Arubaini ya Imam Hussein (A.S).
Habari ID: 2617814    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/12

Kituo cha Kiislamu cha al Azhar nchini Misri kimetoa wito wa kufukuzwa magaidi wote katika nchi za Waislamu.
Habari ID: 2617813    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/12

Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIL) wameharibu misikiti kadhaa na Haram tukufu za Waislamu wa Sunni na Shia katika mkoa wa Salahuddin nchini Iraq.
Habari ID: 2612443    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/28

Tajiri maarufu wa Saudi Arabia Al Waleed bin Talal amekiri kuwa nchi hiyo ya kifalme inawasaidia magaidi wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL) ambalo linapigana dhidi ya serikali za Iraq na Syria.
Habari ID: 1463446    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/25

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina imani kwamba, wale wanaodai kuendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIL) katika eneo wana nia ya dhati juu ya suala hilo.
Habari ID: 1463061    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/22

Waziri Mkuu mteule wa Iraq Haider al—Abadi ni msomi mashuhuri wa Qur'ani.
Habari ID: 1439232    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/14

Jumiya ya Nchi za Kiarabu hatimaye imetoa tamko la kulaani jinai zinazofanywa na kundi la kigaidi la Daesh baada ya kimya cha muda mrefu.
Habari ID: 1438344    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/11

Magaidi wa Kiwahabbi wa kundi la kitakfiri la Daesh wamelibomoa na kubakia kifusi kaburi la Nabii Yunus AS lililoko katika mji wa Mosul, nchini Iraq.
Habari ID: 1433174    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25

Msomi wa Misri mwenye makao yake Qatar Sheikh Yusuf Qardhawi ametangaza kupinga tangazo la matakfiri wa Daesh la kuanzisha kile wanachokiita eti ni 'Khilafa' au utawala wa Kiislamu katika maeneo waliyoyateka Iraq.
Habari ID: 1426193    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/06

Magaidi wa kitakfiri kutoka kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Iraq na Sham (Daesh) wamebomoa misikiti na maeneo kadhaa matakatifu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni katika mkoa unaokumbwa na vita wa Nainawa nchini Iraq.
Habari ID: 1426174    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/06

Ayatullah Khatami
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema, 'kundi la kigaidi la Daesh ni silaha mpya ya Marekani na madola mengine ya kibeberu inayotumiwa kwa lengo la kuvuruga usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.
Habari ID: 1422882    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/27

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga uingiliaji wa Marekani na madola mengine katika masuala ya ndani ya Iraq.
Habari ID: 1421482    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/23

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Waislamu la Iraq litafanikiwa kuwarudisha nyuma magaidi na waungaji mkono wao kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu itafanya kila iwezalo kulinda maeneo matakatifu nchini Iraq.
Habari ID: 1420250    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/19

Ayatullah Ali Sistani, kiongozi mkuu wa kidini wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq amewataka raia wa nchi hiyo kujiepusha na aina yoyote ya hatua za kidini au ukabila zinazoweza kuvunja umoja wao sambamba na kuacha matumizi ya silaha kinyume cha sheria.
Habari ID: 1418402    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/16

Harakati za kundi la kigaidi la DAESH katika maeneo mbalimbali ya Iraq zimekuwa sababu ya mshikamano na umoja kati ya makundi mbalimbali ya taifa la nchi hiyo.
Habari ID: 1417080    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/06/13