IQNA

Arbaeen 1445

Kongamano la wanaharakati wa elimu ya Kiislamu kufanyika Karbala

20:34 - August 26, 2023
Habari ID: 3477499
KARBALA (IQNA) – Kongamano la kwanza la wanaharakati katika uwanja wa Elimu ya Kiislamu litafanyika katika mji mtakatifu wa Karbala wakati wa msimu wa Arabeen.

Kongamano ambalo limepewa jina la "Tunajenga Ustaarabu wa Mahdavi na Shule za Husseini", litaandaliwa na taasisi ya kimataifa ya Noor Mobin kwa ushirikiano na  Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran (ICRO) na asasi kadhaa za kiserikali na za mashinani za Iran na Iraq.

Hujjatul Islam Ali Asghar Mohammadidoust, mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ameliambia Shirika la Habari la IQNA kuwa tukio hilo linaenda sambamba na juhudi za kuanzisha shule za Kiislamu na vituo vya elimu, kukuza elimu kwa mtazamo wa Uislamu na kukuza nafasi yake katika kuendeleza jamii na katika jengo la ustaarabu.

Alisema waanzilishi, wakuu na walimu wa shule za Kiislamu, wanaharakati na wale wanaofanya kazi katika fani ya elimu ya Kiislamu katika nchi tofauti za Kiislamu wahutubia mkusanyiko huo na matokeo yake yatawanufaisha wanafunzi na familia zao.

Aidha ameongeza kuwa, elimu ya Kiislamu ina maana ya kulea kizazi cha baadaye kwa kuzingatia kanuni na mbinu za Kiislamu na kuendesha shule na vituo vya elimu kwa kufuata njia iliyoelezwa katika kazi za Ustadh Shahid Motahhari.

Hujjatul Islam Mohammadidoust amebainisha kuwa katika msimu wa Arbaeen na katika barabara kati ya Najaf na Karbala kuna programu tofauti za kiutamaduni na kielimu kwa mahujaji lakini mkusanyiko huu ni maalum kwa wale wanaohusika na elimu ya Kiislamu na katika kuendesha shule za Kiislamu.

Wanaharakati hao kutoka sehemu mbalimbali za dunia watakutana na kubadilishana uzoefu wao katika nyanja ya elimu ya Kiislamu, alisema.

Kongamano hilo litafanyika katika moja ya shule kuu za mji mtakatifu wa Karbala, alisema, akiongeza kuwa sekretarieti ya kudumu ina jukumu la kupanga kwa tukio hilo kuu.

Moja ya programu kuu wakati wa mkutano huo ni kongamano lililopangwa kufanyika Jumatatu, Septemba 4, pamoja na kushirikisha wanaharakati wa elimu ya Kiislamu wa Iraq, alibainisha.

Pia kutakuwa na maonyesho yanayojumuisha shughuli za shule za Kiislamu na vituo vya elimu, kulingana na mhubiri huyo.

Aidha alisema ili kufikia jamii ya Mahdavi na ustaarabu wa Kiislamu, watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 18 wanapaswa kusoma katika shule ambazo mazingira yake yamejaa mapenzi kwa Imam Hussein (AS) na Ahl-ul-Bayt (AS).

Kwa maelezo zaidi kuhusu mkusanyiko, ingia kwenye https://ifoiet.com/en

3484926

Habari zinazohusiana
captcha