IQNA

11:55 - September 21, 2021
News ID: 3474322
TEHRAN (IQNA)- Kituo kimoja cha Qur’ani nchini Iraq kinatoa mafunzo ya qiraa sahihi ya Qur’ani tukufu kwa wanaoshiriki katika matembezi na ziara ya siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa Sheikh Jawad al Nasrawi, mkurugenzi wa  Taasisi ya Mafundisho ya Qur’ani Tukufu katika Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS), taasisi hiyo imefunguwa kituo chake cha kwanza katika jimbo la Al Muthanna. Vituo kama hivyo vimefunguliwa katika mikoa ya Diwaniya, Babil, Baghdad, Al Hindiya na Karbala. Vituo hivyo vimekuwa vikifanya kazi kwa wiki kadhaa kwa lengo la kuwahudhumia wale walioanza safari ya mapema kutembea kwa miguu kutoka maeneo yote ya Iraq kwa lengo la kushiriki katika ziyara ya Siku ya Arubaini.

Maadhimisho siku ya Arubaini (Arobaini au Arbaeen) hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Mamilioni ya  watu wa Iraq hutembea kwa miguu kutoka miji yao ya mbali na karibu ili kufika Karbala katika siku hiyo ya Arubaini. Halikadhalika wafanyaziara kutoka nchi mbali mbali hushiriki kwa mamilioni katika hafla hiyo. Mwaka huu kutokana na vizingiti vya corona idadi ya washiriki wa Arubaini inatazamiwa kupungua.

 Siku ya Arubaini ambayo mwaka huu intazamiwa kusadifiana na Septemba 27.


آموزش صحیح خوانی قران به زا‌ئران اربعین برای نهمین سال پیاپی

3998603

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: