Sayyid Mohammad Mojani, mkuu wa Kikundi cha Shughuli za Qur'ani katika Kamati ya Utamaduni ya Makao Makuu ya Arbaeen, alieleza kuwa mwaka huu, msafara wa Qur'ani wa Arbaeen utaelekea nchini Iraq kwa msaada wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Astan Quds Razavi, chini ya jina tukufu la Msafara wa Qur'ani wa Imam Ridha (AS).
Aidha, alieleza kuwa kabla ya kusafiri kuelekea Iraq, wanachama wa msafara walifanya Kikao cha Kisomo cha Qur'ani cha Razavi katika Haram ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran siku ya Alhamisi, Julai 24. Tukio hili liliambatana na kumbukumbu ya siku ya arubaini tangu kuuliwa shahidi kwa makamanda wa Kiirani waliopoteza maisha yao katika vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni mwezi Juni.
Mojani alisema kuwa mpango huo ulihusisha kisomo cha aya kutoka Surah Al-Fath, kisomo cha dua ya Aminullah, na hotuba kutoka kwa masheikh na maprofesa wa vyuo vikuu.
Maombolezo ya Arbaeen, ambayo mwaka huu yanaangukia tarehe 14 Agosti, ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani.
Arbaeen ni kumbukumbu ya siku ya arobaini tangu tukio la Ashura, ambalo ni siku ya kuuawa shahidi kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), yaani Imam Hussein (AS).
Kila mwaka, maelfu ya Mashia kutoka pande mbalimbali za dunia hukusanyika Karbala, mahali alipozikwa Imam Hussein (AS), kwa ajili ya kufanya ibada na maombolezo.
Wafanyaziyara hao, wengi wao wakitokea Iraq na Iran, husafiri kwa miguu umbali mrefu kuelekea mji huo mtukufu.
Iran pia hutuma msafara wa Qur’ani, ujulikanao kama Msafara wa Nuur, kuelekea Iraq wakati wa matembezi ya Arbaeen.
Wanachama wa Msafara wa Nuur kutoka Iran hufanya shughuli mbalimbali za Qur’ani na kidini, ikiwemo usomaji wa Qur’ani, Adhana (wito wa swala), na Tawasheeh (kaswida za Kiislamu), katika barabara kati ya Najaf na Karbala, pamoja na maeneo mengine katika msafara wa Arbaeen.
3493978