IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanawake yanafanyika Dubai

23:26 - October 03, 2022
Habari ID: 3475874
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 6 la Mashindano ya Kimataifa la ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wanawake yanaendelea huko Dubai, nchini UAE.

Mashindano hayo yalianza  Jumamosi kwa kushirikisha wawakilishi kutoka nchi 136 ambapo katika usiku wa kwanza wa mashindano hayo, wawakilishi wa Syria, Nigeria, Bangladesh, Mali na Marekani walionesha vipaji vyao vya Qur'ani.

Usiku wa pili, yaani Jumapili, ilikuwa ni zamu ya wahifadhi Qur'ani kutoka baadhi ya nchi nyingine, zikiwemo Sudan, Kenya, Oman, Visiwa vya Comoro, na Thailand.

Hawa ni washindani waliofanikiwa kuingia hatua kuu ya mashindanoo baada ya kufaulu mitihani ya awali yenye lengo la kuthibitisha sifa zao,

Mashindano hayo yataendelea hadi Jumatano, Oktoba 5, na washindi watatunukiwa katika hafla ya kufunga Ijumaa, Oktoba 7, alisema Ibrahim Bu Milha, mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Kiutamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti wa Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai, (DIHQA).

Alibainisha kuwa washindani ni chini ya umri wa miaka 25 na wahifadhi wa Qur'an nzima na wanapaswa kuwa ujuzi juu ya sheria za Tajweed.

Kulingana na afisa huyo, mshindi wa juu wa shindano hilo atapata zawadi ya pesa taslimu dirham 250,000 huku watakaoibuka wa pili hadi wa kumi wakipewa dirham 200,000 hadi 35,000.

DIHQA kila mwaka huandaa hafla ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.

3480712

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha