IQNA

Qari wa Qur'ani

Qari Khalil Al-Hussary wa Misri alijitambua kama mtumishi wa Qur'ani, asema binti yake

20:42 - November 25, 2024
Habari ID: 3479807
IQNA – Bintiye Sheikh Mahmoud Khalil al-Hussary amesema qari huyo mashuhuri wa Misri daima atajielezea kama mtumishi wa Qur'ani Tukufu.

Yasameen al-Hussary alisema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBC cha Misri kuhusu kwa mnasaba wa mwaka wa 44 tokea alipoaga dunia baba yake.

Amesema babu yake aliota ndoto kabla ya kuzaliwa kwa babake ambapo aliona rundo la zabibu likining'inia mgongoni mwake na watu wakila zabibu hizo.

"Alipouliza tafsiri ya ndoto hiyo, aliambiwa kuwa atapata mtoto wa kiume ambaye ataihifadhi Qur'ani na watu watafaidika na elimu yake."

Yasameen amesema kuwa katika utoto wake, Khalil al-Hussary alikuwa akitembea kilomita 7 kufika kituo cha Qur'ani cha Al-Azhar ili kuhifadhi Qur'ani.

Akiwa njiani alikuwa akisoma Qur'ani Tukufu, amebainisha.

Alimuelezea baba yake kama aliyekuwa na uwezo mkubwa wa usomaji wa Qur'ani na daima alijitambulisha kama mtumishi wa Qur'ani na alijulikana kwa usafi wake wa nia, subira, heshima, na kujitolea, alisema.

“Baba yangu alikuwa qari wa kwanza ambaye, kwa ombi la kikundi cha wahifadhi Qur’ani, alirekodi usomaji Qur’ani yote kwaTarteel. Alikataa kupata malipo yoyote ya kifedha kwa kurekodi usomaji wa Tarteel.

Egyptian Qari Khalil Al-Hussary Considered Himself A Servant of Quran, Says Daughter

Pia alibainisha kuwa baba yake alisoma Qur'ani katika Bunge la Marekani wakati wa safari ya kwenda Marekani akifuatana na ujumbe wa Al-Azhar.

Maisha ya Awali na Elimu

Al-Hussary alizaliwa Septemba 17, 1917, katika kijiji kiitwacho Shobra al-Namla katika Jimbo la Gharbia la Misri. Alitoka katika familia ya kidini na alionyesha kipawa cha ajabu cha kuhifadhi na kusoma Qur'ani tangu akiwa mdogo. Aliingia Shule ya Qur'ani akiwa na umri wa miaka minne na akaweza kuhifadhi Qur'ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka minane. Alianza qiraa kwenye mikusanyiko ya watu akiwa na umri wa miaka 12 na akajiandikisha kwa ajili ya mafunzo katika Msikiti wa al-Badawi huko Tanta.

Baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Al-Azhar huko Cairo na akapata stashahada ya "al-Qira'at al-'Ashr" ('visomo kumi'), ambavyo ni njia kumi za kisheria za kusoma Qur’ani Tukufu. Pia alisoma na kufundisha Hadith, Fiqh, na Tafsir huko Al-Azhar.

Kazi na Mafanikio

Mnamo 1944, Sheikh al-Hussary alianza kwa mara ya kwanza kusoma Qur’ani kwenye redio mnamo Februari 16. Pia alishiriki katika shindano lililofanywa na Redio ya Misri ili kuchagua Qari bora ambapo kati ya washiriki 200 alishika nafasi ya kwanza. Kisha aliteuliwa kuwa msomaji katika Msikiti wa Ahmad al-Badawi huko Tanta na baadaye katika Msikiti Muumba..

Al-Hussary alikuwa Qari wa kwanza kurekodi Qur'an nzima kwa mitindo yote miwili ya kisomo, murattal (tarteel) na mujawwad (tajwid). Sauti  yake imesambazwa sana na husikilizwa na mamilioni ya Waislamu kote ulimwenguni.

Alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Muungano wa Wasomaji Qur'ani mwaka 1968 na aliiwakilisha Misri katika makongamano na mashindano kadhaa ya kimataifa ya Qur'ani.

Kifo na Urithi

Al-Hussary aliaga dunia mnamo Novemba 24, 1980, wakati wa safari ya Kuwait, ambapo alialikwa kusoma Quran kwenye msikiti. Alizikwa nchini Kuwait na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu walioomboleza kifo chake

Al-Hussary alikuwa mtu mkarimu na mnyenyekevu ambaye alijitolea maisha na mali yake katika kuitumikia Qur'ani na kuwasaidia wahifadhi Qur'ani. Alitoa wasia theluthi moja ya mali yake itumike kwa ajili ya sadaka zinazohusiana na Qur’ani.

Usomaji wa Al-Hussary wa Qur’ani umesifiwa na wanavyuoni wengi na wasikilizaji kwa uwazi wake, usahihi na uzuri wake. Sauti na mtindo wake umeathiri vizazi vya wasomaji na wasomaji wa Qur'ani kote ulimwenguni. Anajulikana sana kama bwana wa usomaji wa Qur’ani na chanzo cha motisha na mwongozo kwa Waislamu.

Hapa chini ni qiraa ya Al-Hussary.

  

4250170

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misri qari
captcha