IQNA

Jamii

Magaidi wakufurishaji waongezeka Parachinar; wanawaua Waislamu Mashia

23:17 - December 04, 2024
Habari ID: 3479854
IQNA – Kuenea kwa vikundi vya magaidi wakufurishaji katika maeneo ya mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan kumesababisha mateso kwa jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Parachinar, msomi mmoja wa Kiislamu amesema.

Mahojiano na Hujjatul Islam Ali Taghavi, mhubiri wa kimataifa na mkurugenzi wa kikanda wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa nchini Tanzania, Burundi, na Malawi, yanatoa mwanga juu ya unyanyasaji unaoendelea dhidi ya jamii za Shia huko Parachinar, Pakistan.

Hujjatul Islam Taghavi alifafanua juu ya mizizi ya kihistoria, kisiasa na kijamii ya machafuko ambayo yamekumba eneo hilo.

"Ueneaji wa magaidi wa kundi la Daesh kimsingi umetokea katika mikoa ya mashariki ya Afghanistan na mikoa ya kikabila ya Pakistani, na Parachinar iko katikati mwa eneo hili. Hivyo basi, mazingira yanayozunguka ni makazi ya makundi yenye itikadi kali ya Daesh,” aliiambia IQNA. "Makundi haya, moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja, yana jukumu katika migogoro inayolenga idadi ya watu wa Shia, kwani dhamira yao ya kimsingi imejikita katika mateso na mauaji ya Shia."

Taghavi alihusisha hali ya sasa na sera zilizoanzishwa wakati wa miaka ya 1980, wakati serikali ya kijeshi ya Pakistan iliunga mkono kile kilichotajwa kuwa ni jihadi ya Afghanistan dhidi ya Umoja wa Kisovieti. "Kuenea kwa itikadi ya kitakfiri kulianza katika kipindi hiki, na kusababisha migogoro katika jamii ya Mashia huko Parachinar," alieleza.

Parachinar, eneo lenye idadi kubwa ya Mashia linalopakana na Afghanistan, limezungukwa na Mawahhabi wenye misimamo mikali, na hivyo kuwafanya Mashia wawe  hatarini kwa ghasia, alibainisha.

Mhubiri  huyo aliangazia jinsi mambo ya kijiografia yanavyozidisha mivutano ya ndani. "Madola yanayopenda vita duniani, yameingiwa na hofu kutokana na na ushawishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa Mashia wa Pakistan na hivyo yameunga mkono harakati za magaidi wakufurishaji ili wavuruge umoja na utulivu miongoni mwa Mashia" Taghavi alisema.

Taghavi pia alirejelea shughuli za vikundi vingine vya wanamgambo kama Sipah-e-Sahaba na Taliban wa Pakistani (TTP), ambayo alielezea kuwa muhimu katika vurugu zilizolengwa.

Taghavi alikosoa utawala wa Pakistan, akisema kwamba "wakati jeshi lina nguvu, serikali ni dhaifu," haswa katika maeneo ya pembezoni kama Khyber Pakhtunkhwa, ambapo Parachinar iko.

3490928

Kishikizo: pakistan shia
captcha