IQNA

Kauli ya Abbas Salimi kuhusu mkutano na kiongozi wa Hizbullah

Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa muumini na mtumishi wa Qur’ani Tukufu

20:46 - October 06, 2024
Habari ID: 3479547
IQNA-Mtumishi mkongwe wa Qur’ani Tukufu nchini Iran anaamini kuwa Shahidi Sayyid Hasan Nasrallah alikuwa mfano wa wazi muumini wa Mwenyezi Mungu, kamanda shupavu, muumini wa Qur'ani na mtumishi wa Qur'ani, ambaye alistahiki kuuawa kishahidi.

Abbas Salimi; qari mkongwe na wa kimataifa wa Qur’ani, katika mazungumzo na ripota wa IQNA, akiwa na salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kifo cha kishahidi cha Seyyed Hassan Nasrallah; Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisema: Hassan Nasrallah alikuwa kamanda shujaa, Sayyid ambaye alikuwa na Imani imara kuhusu Qur'ani Tukufu. Hakustahiki chochote isipokuwa kifo cha kishahidi. Alijitoa nafsi yake yote katika njia ya Mwenyezi Mungu. Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa mmoja wa waja wa kweli wa Qur'an na Etrat (AS) na hili ni muhimu sana. Leo, wengi wetu ambao tunafanya kazi katika uwanja wa Qur'an, mara nyingi tunazungumza kinadharia kuhusu maswala ya Qur’ani, wakati Sayyiid Hassan Nasrallah alikuwa mtu wa vitendo. Alikuwa mmoja wa mifano mashuhuri ya watu waaminifu katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambao wote wawili walitoa watoto wake katika njia ya Mwenyezi Mungu.
1987: Mkutano wa kwanza na Sayyid Hassan Nasrallah
Mafanikio ya mkutano wa kwanza na mtu huyu mnyenyekevu na mwenye haiba ulikuwa mwaka 1987. Wakati huo, wakati suala la kuwatuma wasomaji Qur’ani wa Iran katika nchi mbalimbali lilipoandaliwa kwa juhudi za shirika la Darul-Qur'an-ul-Karim, pia nilipata bahati ya kwenda Syria nikiwa na maustadhwatatu wa Qur'ani na kisha tukasafiri tusafiri hadi Beirut na Baalbek.
Ustadh Salimi aliongeza kuwa: Baada ya kutekeleza programu mbalimbali nchini Syria, tulikwenda Beirut, na huko tukashiriki hafla katika msikiti ambao Imam wa Jamaa alikuwa marehemu Allama Seyyed Muhammad Hossein Fadhlullah wakati wa mwezi wa Ramadhani. Wakati huo, Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa mwanafunzi mchanga na Katibu Mkuu wa Hizbullah alikuwa Seyed Abbas Mousavi.
Mwaliko wa Seyyed Hassan Nasrallah wa kutekeleza programu ya Qur'ani katika Siku ya Quds
Salimi alisisitiza kuwa: Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa miongoni mwa wale ambao walifurahishwa sana tulipoandaa hafla na mahafali za Qur'ani. Katika mwaka huo huo, tulialikwa kushiriki vikao vya Qur’ani katika Siku ya Quds huko Lebanon.
Mkutano baada ya miaka 18 katika Haram ya  Hadhrat Abduladhim (AS)
Miaka ilipita tangu mkutano huo hadi mwaka 2005. Wakati huo nilikuwa nikihudumu  katika Haram ya Shah Abd al-Adhim al-Hasani (AS), kusini mwa Tehran. Marehemu Ayatullah Rayshahri alinifahamisha kwamba mgeni maalum atatembelea kaburi hilo lililobarikiwa, naye si mwingine bali ni Shahidi Sayyid Hasan Nasrallah, ambaye nilipaswa kumkaribisha rasmi.
Uso wake ulijaa nuru,  utulivu na umaanawi
Akiashiria kwamba muda mfupi baada ya tukio hili, vita vya siku 33 vya Hizbullah na Israel vilianzishwa na hatimaye kupelekea Israel kushindwa kwa fedheha, Salimi alisema: Uso wa Sayyid ulijaa nuru, utulivu na umaanawi. Ameongeza kuwa: “Nina furaha sana kwamba katika amri ya Amiri Jeshi Mkuu baada ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ilisisitizwa kwamba harakati hii ya muqawama haitasitishwa kwa njia yoyote ile, kama vile bendera ya Uislamu imekuwa ikipepea katika hali zote kwa muda wa miaka zaidi ya 1400."

/4239614

Habari zinazohusiana
captcha