Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) Palestina, Hamas, imesema: "Tunabariki urushaji wa makombora ya Iran ambayo yalikuja kujibu hujuma ya Wazayuni dhidi ya watu wa Palestina na Lebanon.
"Tunathibitisha kwamba jibu hili la heshima la Iran ni ujumbe mzito kwa adui Mzayuni na serikali yake ya kifashisti. Operesheni hii ina lengo la kuzuia na kudhibiti ugaidi wa Wazayuni. Jinai, kiburi na ukiukaji wao wa sheria za kimataifa na kanuni za kibinadamu umevuka mipaka yote."
“Tunadhihirisha fahari yetu kwa ndugu zetu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na shukrani zetu kwa misimamo yao dhidi ya kiburi kisichozuiliwa cha Wazayuni.” Taarifa hiyo pia imeipongeza Iran kwa kujifungamanisha na maadili ya uadilifu, mapambano ya watu wa Palestina, watu wa Lebanon, pamoja na maslahi makuu ya umma wa Kiislamu.
Mwishowe, taarifa hiyo imezitaka nchi zote, watu, vyama na nguvu zote za mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kusimama kidete na kukabiliana na jinai za Wazayuni na mradi wa kupenda kujitanua wa Kizayuni unaolenga kila mtu.
"Tunawahimiza jitihada za kila aina ili kukomboa ardhi yetu na matukufu yetu kutoka kwa uchafu wa uvamizi wa fashisti."
Kamati ya Uratibu wa Mapambano ya Kiislamu nchini Iraq pia imetoa taarifa.
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Iwapo Wamarekani wataingilia hatua yoyote ya uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu au adui wa Kizayuni akitumia anga ya Iraq kutekeleza mashambulizi yoyote ya mabomu katika ardhi ya Iran, basi maeneo yote ya Marekani nchini Iraq na eneo hilo yatakuwa shabaha yetu na hawataweza kutoroka”.
Naye Msemaji wa Ansarullah ya Yemen Mohammed Abdul Salam amesema: "Kuzuia na kukabiliana na kundi la adui wa Kizayuni ndiyo njia pekee ya kuzuia kuendelea na jinai zake za kinyama dhidi ya wananchi wa Palestina na Lebanon na katika eneo hili."
"Tunabariki operesheni ya Iran iliyolenga shabaha za kijeshi za adui ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel), na tunaipongeza Jamhuri ya Kiislamu kwa uungaji mkono wake kwa Palestina na muqawama wake dhidi ya himaya ya Marekani katika eneo."
4240058/