Ilizinduliwa katika Msikiti wa Al-Manshiyah katika eneo la Siwa la Mkoa wa Marsa Matrouh.
Sheikh Hassan Muhammad Abdul Basir Arafa, mwakilishi wa Wizara ya Wakfualizindua shule ya Qur'ani katika hafla iliyohudhuriwa na wanafunzi 200 wa Qur'ani.
Mpango huo ni sehemu ya juhudi za kutekeleza maagizo ya Waziri wa Wakfu Usama Al-Azhari, yenye lengo la kuzihuisha shule za Qur'ani kote nchini.
Sheikh Arafa alisema kuwa mpango wa kutoa mafunzo kwa wahifadhi 100 wa Qur'ani kila mwaka utadumu kwa muda wa miaka mitano na kutakuwa na sherehe za kuhitimu kila mwaka.
Mpango wa kufufua shule za Qur'ani utaepelekea kuundwa kwa mazingira yenye afya kwa vijana na elimu yao ifaayo kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani "ambayo mababu na wasomi wetu walilelewa," alisema.
Kuimarisha uhusiano wa kizazi kipya na Qur'an na mafundisho yake kwa kuwaongoza kwenye Qur'an, kusoma, na kutekeleza hadithi ya Mtume SAW isemayo "Bora miongoni mwenu ni wale wanaojifunza Qur'an na kuifundisha" ni miongoni mwa malengo ya mpango huu, alibainisha.
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.
Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani zimeenea sana katika nchi hiyo ya Kiarabu yenye Waislamu wengi na wengi wa makari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu hapo awali na wa sasa wamekuwa Wamisri.
3491137