Jumuiya hiyo imewataja na kuwaonya maqari hao watano kuwa ni Ahmed Naji Shahin, Madhat Marei, Ahmed al-Suaidi, Ismail al-Tabbakh na Farid Asil.
Jumuiya hiyo imesema wameisoma Qur'ani kwa mitindo isiyo na heshima na isiyo sahihi jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Wakati huo huo, Mufti Mkuu wa Misri Nazir Mohamed Ayyad amelaani vitendo vya kusikiliza usomaji wa Quran sambamba na uchezaji wa ala za muziki.
Alisema ni dhambi kubwa kwani Mafaqihi wa Kiislamu wamesema vitendo hivyo ni udhalilishaji wa hadhi ya Qur'ani Tukufu. Wakati huo huo, wasomaji kadhaa wa Qur'ani wa Misri hivi karibuni wamesimamishwa kazi au kupigwa marufuku kwa kufanya makosa wakati wa kusoma Kitabu Kitukufu.
Jumuiya hiyo imewataka maqari kufanya mazoezi na kujiandaa kikamilifu kabla ya kusoma Qur'ani katika hafla za umma au kwenye vyombo vya habari.
3490826