Amesema kuwa timu ya IRCS ilikamilisha kuandaa kwa vifaa vyote hospitali ya muda huko Arafat kabla ya Siku Tukufu ya Arafah, inayotarajiwa kuwa Alhamisi.
Mbali na hospitali hizo za muda Arafat na Mina, Koulivand ameeleza kuwa hospitali ya IRCS mjini Makkah inaendelea kutoa huduma za kiafya na matibabu kwa mahujaji.
Akizungumzia kuhusu uundwaji wa “Msafara Maalumu wa Dharura kwa Wuquf,” amesema kuwa kwa Mahujaji wenye hali maalumu za kiafya wanaohitaji msaada wa ziada, msafara maalum umeandaliwa ili kuhakikisha ibada zao za Hija zinafanyika kwa usahihi chini ya usaidizi wa madaktari na wataalamu wa afya.
“Wagonjwa wote waliolazwa hospitalini wataweza kutekeleza ibada zao kwa mujibu wa masharti ya dini, kwa msaada wa timu za afya,” amesema Koulivand.
“Tuna matumaini kuwa siku hizi tukufu zitapita salama kwa uwepo madhubuti wa wahudumu wa afya wa Hilali Nyekundu. Kwa kutumia rasilimali zetu zote, vifaa vyetu, na uratibu wa hali ya juu, tumesimama bega kwa bega na mahujaji katika kulinda afya na maisha yao.”
3493328