IQNA

Seneta wa Marekani aonya kuhusu kushadidi Chuki dhidi ya Uislamu kabla ya Mwezi wa Ramadhani

17:32 - January 14, 2026
Habari ID: 3481802
QNA – Mwanasiasa mmoja wa Marekani ameonya kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani unakaribia.

Seneta Mark Warner alisema katika hotuba yake kwenye Seneti ya Marekani kuwa kauli na vitendo vya baadhi ya maafisa vimezidisha mazingira ya uhasama dhidi ya jamii za Waarabu na Waislamu.

Alionya kuwa matamshi ya kisiasa yanayolenga Waislamu yanaweza kuchochea zaidi kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu katika jamii za Magharibi.

Warner alirejea matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa hivi karibuni dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Somalia, akisema kauli hizo zimezua wasiwasi miongoni mwa Waislamu kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa vurugu na uhalifu wa chuki dhidi yao nchini Marekani na Ulaya.

Aliwataka wanasiasa wote kulaani kwa uthabiti na bila kusitasita aina zote za ubaguzi wa kidini na kikabila.

Habari inayohusiana:

Alisisitiza kuwa juhudi za kupambana na ubaguzi na ubaguzi wa rangi zinapaswa kuendelea wakati wote na zisibaki tu wakati wa matukio maalum, akibainisha umuhimu wa mashirika ya kiraia na taasisi za elimu katika kukuza thamani za uvumilivu na kuishi kwa amani.

Masuala ya chuki dhidi ya Uislamu na haja ya kuyakabili yamekuwa mjadala wa kawaida katika jamii nyingi za Magharibi katika miaka ya karibuni.

3496058

Habari zinazohusiana
captcha