IQNA

Kipindi maalumu cha Ramadhani kitatayarishwa katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) jijini Cairo

15:04 - February 16, 2026
Habari ID: 3481944
IQNA – Kipindi maalumu cha Qur'ani kwa ajili ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kinatarajiwa kutayarishwa na mwanaharakati wa vyombo vya habari wa Misri, Amr Al‑Laithi.

Amr Al‑Laithi, mtangazaji mashuhuri wa Misri, atakuwa mtangazaji mkuu wa kipindi hicho, ambacho kitarushwa mubashara kutoka Msikiti wa Imam Hussein (AS) mjini Cairo.

Kipindi hicho kitaendeshwa katika uwepo wa kundi la masheikh mashuhuri, wasomaji wa Qur'ani (maqari), pamoja na wasomaji wa Ibtihal (dua na nyimbo za kumsifu Mwenyezi Mungu), katika mazingira ya kipekee yaliyojaa unyenyekevu na hali ya kiroho.

Mpango huo maalumu utajumuisha mahojiano na idadi ya maqari wanaoongoza Swala za Taraweeh, ambazo ni miongoni mwa ibada zilizosisitizwa kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni katika mwezi wa Ramadhani, wakati wa usiku wa Ramadhani katika msikiti huo. Aidha, kutakuwa na vipengele vya kidini vinavyozungumzia fadhila za mwezi mtukufu, njia za maandalizi ya kiroho, na namna bora ya kunufaika na baraka za funga.

Habari inayohusiana:

 
 

Miongoni mwa malengo ya uzalishaji wa kipindi hiki ni kusikika kwa tilawa za Qur'ani Tukufu na dua kutoka kwa wasomaji mashuhuri wa Ibtihal, pamoja na kuandaa mazingira maalumu ya kiroho yanayoakisi undani na nuru ya mwezi wa Ramadhani.

Kipindi hiki kinatarajiwa kurushwa kupitia mtandao wa televisheni ya satelaiti ya Misri, Al‑Hayat, kama sehemu ya ratiba yake maalumu ya vipindi vya Ramadhani.

3496429

captcha