IQNA

Wahudumu wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbalikuenziwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran

15:14 - February 20, 2026
Habari ID: 3481961
IQNA – Mkurugenzi wa sehemu ya kimataifa ya Maonyesho ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaTehran amesema kuwa kuwaenzi wahudumu wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali kutakuwa miongoni mwa programu kuu za sehemu hii ya kimataifa.

Aidha, sehemu hiyo pia itaandaa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 1,500 ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW). Haya yamesemwa na Hujjatul-ul-Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshabouri, ambaye pia ni mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Qur’ani na Da‘wah chini ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran, katika mahojiano na IQNA kabla ya ufunguzi wa maonyesho hayo.

Maonyesho ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yatafunguliwa rasmi katika Msikiti wa Imam Khomeini (RA) – Mosalla ya Tehran siku ya Jumapili, Februari 22, 2026, na yataendelea hadi Machi 6, chini ya kaulimbiu isemayo: “Iran chini ya Ulinzi wa Qur’ani.”

Swali: Sehemu ya kimataifa ya maonyesho itaanza lini na itaendelea kwa muda gani?

Jibu: Ufunguzi wa sehemu ya kimataifa utafanyika sambamba na ufunguzi wa sehemu ya ndani ya nchi. Hii ina maana kuwa sehemu ya kimataifa itaanza tangu siku ya kwanza ya maonyesho.

Kwa hivyo, sehemu hii itaanza siku ya tatu ya Ramadhani na itaendelea kwa wiki mbili kamili.

Swali: Ni nchi ngapi zitashiriki, na kwa aina gani za kazi na bidhaa?

Jibu: Mwaka huu, nchi shiriki zitahusika katika sekta tatu:

  • kazi za kisanaa,
  • kisayansi,
  • na bidhaa za kitamaduni.

Takribani nchi 10, zikiwemo Uturuki, Oman, Misri na Bahrain, zitashiriki katika sekta ya sanaa, huku nchi saba zikishiriki katika sekta ya kisayansi.

Aidha, nchi tatu zitawasilisha kazi za kitamaduni zenye mada za Qur’ani. Kwa jumla, nchi 20 zitashiriki katika tukio hili.

Swali: Je, utofauti wa kijiografia na kitamaduni umezingatiwa katika kualika nchi?

Jibu: Tumetoa uzito maalumu kwa suala la utofauti. Washiriki kutoka mabara na maeneo mbalimbali watakuwepo, ikiwemo nchi za Afrika na Afrika Kaskazini, ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, nchi jirani, Indonesia, nchi za ASEAN, pamoja na bara Hindi.

Swali: Je, kutakuwa na sherehe maalumu za ufunguzi na ufungaji kwa sehemu ya kimataifa?

Jibu: Hapana. Sehemu ya kimataifa itafunguliwa na kufungwa kwa pamoja na sehemu ya ndani ya nchi, hivyo hakutakuwa na sherehe tofauti au huru kwa sehemu hii.

Swali: Ni programu zipi zitakazofanyika katika sehemu ya kimataifa? Je, kutakuwa na mikutano na semina kama miaka iliyopita?

Jibu: Mwaka huu, tutashuhudia mipango na shughuli mpya kwa mara ya kwanza katika sehemu ya kimataifa.

Mbali na kuwaenzi wahudumu wa Qur’ani wa ndani ya Iran, wanazuoni na wahudumu mashuhuri wa Qur’ani kutoka nje ya Iran pia wataenziwa, kwa ushirikiano na Baraza Kuu la Qur’ani, Makao Makuu ya Kuheshimu Wahudumu wa Qur’ani, na Tume ya Maendeleo ya Shughuli za Kimataifa za Qur’ani.

Waheshimiwa hawa wamependekezwa kutoka nchi mbalimbali. Aidha, kutakuwa na takribani uzinduzi 20 wa kazi mpya na vikao 20 vya mijadala katika sehemu ya kimataifa.

Swali: Ni kipengele gani muhimu zaidi kitakachotofautisha sehemu hii na miaka iliyopita?

Jibu: Miongoni mwa mambo mapya ni kuwasilisha uwezo na mchango wa Qur’ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia video (clips) na vijitabu katika lugha mbalimbali kwa wageni wa kimataifa.

Pia, Mkutano wa Nne wa Qur’ani wa Tehran utafanyika, ambapo wanazuoni wa Qur’ani kutoka nchi mbalimbali watawasilisha tafakuri na mihadhara yao juu ya mada:

“Qur’ani na Mtume (SAW)”, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 1,500 ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (SAW).

Swali: Je, kuna mgeni maalumu au shughuli mpya mwaka huu?

Jibu: Mgeni maalumu wa sehemu hii ni Sheikh Abu Jarrah Soltani, msomi wa Qur’ani kutoka Algeria, ambaye ameandika juzuu 25 za tafsiri ya Qur’ani. Wageni wengine kadhaa pia wanatarajiwa.

Swali: Kwa kuwa maonyesho haya yanazingatia Qur’ani, Nahj al-Balagha na Sahifa Sajjadiyya kwa pamoja, hili litazingatiwa vipi katika sehemu ya kimataifa?

Jibu: Masuala ya Etrat (Ahl-ul-Bayt AS), yakiwemo Nahj al-Balagha na Sahifa Sajjadiyya, hayatenganishwi na Qur’ani. Maonyesho haya ni ya Qur’ani na Etrat kwa pamoja.

Habari inayohusiana:

Kuna wanaharakati na watafiti nje ya Iran wanaopenda Qur’ani na Ahl-ul-Bayt (AS), na wamefanya kazi juu ya dhana za pamoja katika uwanja huu. Wengine wamejihusisha na kufafanua mafundisho ya Qur’ani kupitia njia ya Ahl-ul-Bayt (AS), wakijikita katika Nahj al-Balagha na Sahifa Sajjadiyya, na kazi zao zitajadiliwa katika toleo hili.

Aidha, tutashuhudia uzinduzi wa kazi mpya, hususan zile zinazozingatia mada kama jihadi ya ufafanuzi, uhamsishaji wa fikra, kupambana na maadui, vita laini (soft war), na vita vya simulizi (war of narratives).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, yakiratibiwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran.

Kupitia programu mbalimbali kama vikao maalumu, warsha za kielimu, vikao vya Qur’ani, na shughuli mahsusi kwa watoto na vijana, tukio hili linalenga kueneza mafundisho na utamaduni wa Qur’ani.

Maonyesho haya pia ni jukwaa la kuonesha mafanikio mapya ya Qur’ani nchini Iran, pamoja na bidhaa na kazi mbalimbali zinazolenga kuutumikia na kuukuza Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

 

4335267

Habari zinazohusiana
captcha