Katika taarifa ya karibuni, Al‑Azhar ililaani mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran dhidi ya kambi za kijeshi za adui ambazo zimejengwa katika baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi.
Ikijibu taarifa hiyo, Taasisi ya Qur’ani ya Noon nchini Yemen ilisema kuwa kauli hiyo imejitenga na misingi ya Qur’ani Tukufu inayohimiza kulindwa na kudhihirishwa kwa haki.
Taasisi hiyo ilisisitiza umuhimu wa kutambua hatari ya kauli zinazotolewa bila kuzingatia muktadha wake, huku chanzo na mizizi ya mgogoro ikipuuzwa.
Iliongeza kuwa: “Kauli za namna hii, iwe zimetolewa kwa makusudi au bila kukusudia, zinafanya wale wanaofanya uadui na uvamizi kuwa sawa na wale wanaolinda taifa lao na heshima yake.”
Katika taarifa yake, taasisi hiyo ilisema pia: “Hali ya sasa inayolikumba Umma wa Kiislamu si hali ya kauli za haraka au maoni ya kupita. Ni hali ya kutofautisha wazi kati ya misimamo inayowaunga mkono waliodhulumiwa na ile inayodhoofisha uwepo wa haki katika fikra na uelewa wa jamii.
Kwa hiyo ni wajibu haki ielezwe kikamilifu, kwa kutegemea Kitabu cha Mwenyezi Mungu, bila kushinikizwa wala kupendelea upande fulani, na kwa kuzingatia mizani thabiti ya uadilifu.
Kwa sababu hii, tumekuwa waangalifu tunapowahutubia wanazuoni wa Al‑Azhar, tukiwa katika msimamo wa jukumu la kidini, si wa uadui, na kuwakumbusha kuwa wanapaswa kusema kwa uadilifu, kama Allah anavyosema:
“…Mnaposema, semeni kwa uadilifu…” (Al‑An‘ām: Aya 152).
Tunaukosoa msimamo wa Al‑Azhar juu ya matukio ya eneo hili, na namna ilivyoitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa mhusika wa uadui, bila kutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu muktadha mzima wa mgogoro, wala kubainisha wazi tofauti kati ya uadui uliokatazwa na utetezi halali.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu, tunasisitiza kuwa vita katika Uislamu si ruhusa ya kufanya uadui kiholela, bali ni njia ya kuondoa dhuluma na kulipiza kisasi kwa uadui uliofanywa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
“Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa.”
Kulenga kambi au vituo vya kijeshi vya Marekani vinavyotumika katika mashambulizi dhidi ya nchi za Kiislamu ni jambo lililo mbali kabisa kisheria na kimaadili na kulenga raia wasio na hatia. Hili linapaswa kuelezwa kwa uwazi katika mazungumzo ya kifiqhi na kisheria za Kiislamu.
Tunasisitiza pia kuwa utukufu wa damu ya raia ni kanuni isiyopingika, na ni kipimo tunachotumia kupima matendo yote bila upendeleo wala mapendeleo ya upande wowote. Uadilifu unatukalifisha kutofautisha kati ya wanaolenga vituo vya kijeshi na wale wanaopanua madhara kwa kuwalenga raia wasiokuwa na hatia.
Nafasi ya Al‑Azhar katika dhamiri ya Umma inataka iwe sauti ya kuunganisha, si chombo cha kutengeneza fitina ; iwe mizani ya uadilifu, si kioo kinachoakisi shinikizo za kisiasa; na iwe mtoaji wa haki kwa ukamilifu wake, si kwa njia iliyogawika na kuchagua-chagua.
Kwa hivyo, Taasisi ya Qur’ani ya Noon ina hofu kwamba kauli zisizo na uwiano, ambazo hazionyeshi ukweli wote, zitasababisha machafuko katika fahamu za Umma na kudhoofisha imani katika mjadala wa kidini. Hii ni hasa pale ambapo taarifa yenu ya hivi karibuni imejitenga na muktadha kamili ambao Umma umekuwa ukiishi kwa miongo kadhaa, ambapo unashambuliwa na miradi ya kutawala na mashambulizi endelevu, huku kukiwa na mbelepari wa upinzani uliojitokeza kukabiliana na hali hii, ambao unajulikana leo kama “Mhimili wa Muqawama”.
Tunasisitiza kuwa mhimili huu, unaojumuisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wanajionesha wenyewe kama mbelepari dhidi ya uadui na kwa kuunga mkono waliodhulumiwa, hasa katika suala la jukumu la Palestina, tukitegemea kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na Tulitaka kuwapa neema wale waliodhulumiwa katika nchi na kuwafanya wao kuwa viongozi na kuwafanya wao kuwa warithi.”
Aidha, vitendo vyao vya kijeshi, pale vinapoelekezwa dhidi ya kambi na vituo vinavyotumiwa katika uadui, vinakubaliwa na Qur’ani ndani ya mfumo wa utetezi binafsi (kujilinda), na si katika maana ya uadui uliokatazwa, kama Allah Mtukufu anavyosema: “Basi anayekupindukia nyinyi, wapindukieni kwa mfano wa kile alichowapindukia nyinyi.”
Kupuuza kanuni ya kusaidia waliodhulumiwa na kuonyesha vikosi vya Kiislamu kama chanzo cha hatari ni upotofu katika uelewa wa Qur’ani Tukufu.
Kwa hivyo, tunawahimiza kwa dhati kufikiria upya misimamo yenu kwa namna itakayotimiza uadilifu wa kina wa Qur’ani, na kuwasilisha mjadala unaoweka kila tendo katika muktadha wake unaostahili, na kuwashikilia wale wanaofanya uadui.
Tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu:
“Na chuki dhidi ya watu fulani isiwafanye msiwe na wenye kutenda haki.”
Maana maneno, amana, na kauli zote ni ushahidi, na historia haisahau misimamo ya wanazuoni katika nyakati za majanga na shida. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape mwongozo wa kile kinachotegemeza ukweli, kukiunganisha Umma wa Kiislamu, na kutimiza jukumu la kueleza haki kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha.
Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuongoza kwenye Njia Iliyonyooka.
3496905