IQNA

Wawakilishi wa Iran Wang’ara katika Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani ya Karbala

17:47 - June 12, 2026
Habari ID: 3482351
IQNA – Wawakilishi wote wa Iran katika toleo la tano la Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani ya Karbala nchini Iraq wamepata nafasi za juu katika vipengele mbalimbali vya mashindano.

Sherehe ya kufunga tukio hilo la kimataifa la Qur’ani ilifanyika jioni ya Jumatano, tarehe 10 Juni, katika haram takatifu ya Imam Hussein (AS) mjini Karbala.

Kwa mujibu wa jopo la majaji, wawakilishi wote saba wa Iran walikuwa miongoni mwa washindi wa juu.

Katika kipengele cha kuhifadhi Qur’ani Tukufu nzima, Mohammad Laini wa Iran alipata nafasi ya kwanza huku Amir Hossein Attarzadeh akishika nafasi ya tatu.

Katika kipengele cha usomaji wa Qur’ani, Omid Hosseinnejad alipata nafasi ya pili, na Yousef Jafarzadeh akamaliza katika nafasi ya nne.

Katika kipengele cha vijana, Asgarnejad, Najafi na Hosseinzadeh walishika nafasi ya tatu, ya nne na ya tano mtawalia.

Toleo la tano la Tuzo ya Kimataifa ya Usomaji na Hifdhi ya Qur’ani ya Karbala lilianza tarehe 6 Juni katika haram takatifu ya Imam Hussein (AS) na kuhitimishwa usiku wa Jumatano kwa sherehe ya kufunga ambapo washindi bora walitunukiwa.

Wawakilishi kutoka nchi 30 za Kiarabu na Kiislamu walishiriki katika mashindano hayo, wakiwemo wawakilishi saba kutoka Iran.

3497800/

captcha