IQNA

Mkakati wa Kistaarabu wa Umoja wa Imamu Shahidi kwa Ummah wa Kiislamu: Mtazamo wa Msomi wa Bahrain

17:02 - July 10, 2026
Habari ID: 3482465
IQNA – Msomi mwandamizi wa Bahrain amesema kuwa umoja katika mtazamo wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, si nembo tu ya kisiasa; bali ni neno-msingi katika mkakati wake wa kistaarabu wa kurejesha izza, heshima na mamlaka kwa Ummah wa Kiislamu.

Katika mahojiano maalumu na IQNA, Sheikh Abdullah Daqqaq amebainisha vipengele mbalimbali vya mbinu za Kiongozi Shahidi kuelekea umoja wa Waislamu.

Amesema kuwa Imamu Shahidi aliuona umoja wa Kiislamu kama wajibu wa kidini na hitaji la kimkakati na kistaarabu kwa Ummah, na wala si mbinu ya muda mfupi ya kisiasa.

“Amesisitiza kuwa maadui wa Uislamu wanauyumbisha Ummah wa Kiislamu kama chombo kimoja na hawafanyi tofauti kati ya madhehebu mbalimbali; kwa hivyo, kukabiliana na changamoto za kisiasa, kijeshi, na kiutamaduni kunawezekana tu kupitia umoja wa Waislamu, mshikamano wao katika mhimili wa mambo ya msingi wanayoshirikiana, na kuepuka mifarakano, jambo ambalo litaimarisha uwezo wa Ummah wa Kiislamu.”

Ameongeza kuwa Shahidi Ayatullah Khamenei alizingatia mambo yafuatayo kuwa ni vizuizi vikuu vya ukaribu (Taqrib) na umoja wa Kiislamu:

a) Misimamo mikali ya kidini au kimadhehebu na taasubi za kimadhehebu: Alikiona kipengele hiki kuwa kizuizi kikubwa cha ndani kwa umoja wa Kiislamu, akisema: ‘Kuna kizuizi cha ndani cha umoja, nacho ni taasubi za kidini. Taasubi hizi zipo katika dini zote na lazima ziondolewe.’ Alisisitiza kuwa kushikamana na imani ya madhehebu ni jambo la halali, lakini tatizo huanza pale utetezi wa madhehebu unapogeuka kuwa uadui dhidi ya madhehebu mengine au kutukana matukufu yao.

b) Kuchochea tofauti za kimadhehebu na kihistoria hadharani: Alitofautisha kati ya utafiti wa kielimu na uchochezi wa hisia za umma.

c) Miradi ya kiistikbari na kikoloni: Miradi inayofuatiliwa kwa lengo la kuugawa na kuusambaratisha Ummah wa Kiislamu. Miongoni mwa kauli zake maarufu ni: ‘Maadui wa Ummah wa Kiislamu wanataka kuweka umbali kati ya Iran na ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na baina ya Waislamu wenyewe.’

d) Mienendo ya Takfiri na ya kigaidi: Ayatullah Khamenei alikiona kitendo cha kufurishana (Takfir) kuwa ni chombo hatari zaidi cha kuugawa Ummah. Alisema: ‘Mienendo ya Takfiri kwa vitendo inatumikia malengo ya mabeberu (uistikbari), serikali za kikoloni, na utawala wa Kizayuni, ijapokuwa wanafanya kazi chini ya kivuli cha Uislamu.’

e) Kutozingatia maslahi ya pamoja: Kughafilika na maslahi makuu ya Ummah na kushughulishwa na migogoro midogo isiyo na tija.

Sheikh Daqqaq amebainisha kuwa mapambano dhidi ya migawanyiko ya kimadhehebu na fitna yalichukua nafasi ya kati katika hotuba na jumbe za Ayatullah Khamenei. Amesisitiza mara kwa mara kuwa kuchochea migogoro ya kimadhehebu ni miongoni mwa miradi hatari zaidi inayolenga ulimwengu wa Kiislamu, na kwamba kulinda umoja wa Ummah ni moja ya majukumu muhimu zaidi ya kidini na kisiasa katika zama hizi.

Amesisitiza daima kuwa umoja haumaanishi kuunganisha madhehebu au kufuta sifa zao za kiitikadi na kifiqhi, bali inamaanisha kukubaliana juu ya maslahi makuu ya Ummah wa Kiislamu na kufanya kazi pamoja kuyatetea.

Imamu Khamenei aliamini kuwa izza, uhuru, na maendeleo ya kisayansi, kisiasa na kiuchumi ya Ummah wa Kiislamu yanategemea umoja na mshikamano wake, na kwamba migawanyiko inapelekea kupotea kwa uwezo na kudhoofisha uwezo wa kukabiliana na changamoto za nje; huku umoja ukitoa fursa ya kutumia uwezo mkubwa wa mataifa ya Kiislamu katika njia ya maendeleo.

Alipoulizwa kuhusu hatua alizochukua Kiongozi Shahidi kufanikisha ukuruba na umoja wa  wa madhehebu ya Kiislamu, Sheikh Daqqaq alisema:

Miongoni mwa hatua na mikakati muhimu ambayo Imamu Khamenei aliunga mkono ni:

  • Kuunga mkono mazungumzo ya kielimu na mikutano kati ya wanazuoni wa madhehebu mbalimbali.
  • Kuimarisha shughuli za Jumuiya ya Kimataifa wa Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu (World Forum for Proximity of Islamic Schools of Thought).
  • Kusisitiza juu ya marufuku uharamu) wa kutukana alama na matukufu ya madhehebu ya Kiislamu.
  • Kuimarisha “Wiki ya Umoja wa Kiislamu” kama fursa ya kuimarisha muungano miongoni mwa Waislamu.
  • Kusisitiza kuhusu masuala makuu ya Ummah, hususan suala la Palestina.

Sheikh Daqqaq pia aliulizwa kuhusu nafasi ya wanazuoni na wasomi wa kidini katika kufikia umoja. Alisema:

Shahidi Ayatullah Khamenei aliamini kuwa wanazuoni wana jukumu kubwa ambalo linatekelezwa kupitia:

  • Kukuza utamaduni wa kuheshimiana kati ya wafuasi wa madhehebu tofauti.
  • Kuepuka lugha za uchochezi na tabia zinazosababisha fitna.
  • Kusisitiza juu ya imani, fiqhi, na staarabu zinazoshirikishwa.
  • Kuwaamsha watu kuhusu hatari ya miradi ya Magharibi na Uzayuni inayolenga kuugawa na kuusambaratisha Ummah wa Kiislamu.
  • Kupanua uhusiano wa kielimu na kiutamaduni kati ya taasisi mbalimbali za kidini.

3498185

captcha